Na.Joseph
Ngilisho,Arusha
Ukistajabu ya
Mussa, utapata ya Firauni,mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu
(jina linahifadhiwa),mkazi wa Sokoni One jijini hapa, amebakwa na kunajisiwa na
mwanamme mwenye umri wa miaka 30.
Mtuhumiwa ametajwa
kwa jina la Rajabu Mkoba, mkazi wa eneo hilo.
Ilidaiwa mtuhumiwa alimbaka
mtoto huyo kwa zaidi ya saa 9 baada ya kumchukua kwa mtu aliepewa kumtunza.
Tukio hilo lilitokea
Agosti 3 mwaka huu huku mama mzazi wa mtoto huyo, Mwitango Yambazi Mtalu (27), akishindwa
kutoa taarifa polisi baada ya kuahidiwa shilingi 100,000.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi, mama wa mtoto huyo, alisema siku ya Jumapili majira
ya asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la
Mustafa Kabananga, ili apate nafasi ya kushiriki mkutano wa kikundi chake.
Alisema baada ya
kurudi jioni majira ya saa mbili usiku alikwenda kwa jirani yake huyo kwa lengo la
kumchukua mtoto wake lakini aliarifiwa mtoto wake alichukuliwa na kijana
aliyemtaja kwa jina la Rajabu ambaye anafahamika eneo hilo.
Alisema aliamua
kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa ambaye anaishi na wazazi wake, hata hivyo
hakufanikiwa kumkuta wala mtoto wake na kurejea nyumbani huku akiendelea na
jitihada za kumtafuta.
Alisema aliamua
kwenda kituo cha polisi Unga Limited kumuulizia akiongozana na balozi wa nyumba
kumi.
Hata hivyo, polisi
walimtaka arudi nyumbani hadi asubuhi arejee kituloni kwa ajili ya taratibu nyengine.
Alisema wakati
akirejea nyumbani majira ya saa 9 usiku alimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa
aliyetambukika kwa jina la mama Mkoba akiwa na mtoto wake akimrejesha huku
mtuhumiwa akiwa hayupo.
Baada ya kukabidhiwa
aliamua kumchunguza vizuri ndipo alipokuta sehemu za siri za mtoto wake
zimevimba kupita kiasi huku damu ikitoka mara kwa mara.
Aliamua kumweleza
mama wa mtuhumniwa jinsi mtoto wake alivyoharibiwa, ambapo mama huyo alimsihi asitoe
taarifa popote na kwamba atampatia shilingi 100,000 na kumpeleka mtoto huyo
hospitali.
Hata hivyo, mama wa
mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo, hakumpeleka hospitali yeyote badala
yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.
Lakini baadhi ya
majirani walikerwa na kitendo cha mama wa mtoto kunyamazia unyama huo ndipo walipomvamia
kwa maneno makali na kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.
Kufuatia kelele za
majirani ndipo alipokubali kwenda kituo cha polisi Unga Ltd ambapo polisi
walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kumpeka
hospitali ya Mount Meru.
Mama wa mtoto huyo
na wa mtuhumiwa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano huku mtuhumiwa akiendelea
kusakwa.
No comments:
Post a Comment