Habari za Punde

Polisi Zanzibar Yamshikilia Mtuhuma wa Ujambazi

Na.Khamisuu Abdallah
JESHI la Polisi linamshikilia mtu mmoja kwa kudaiwa kuhusika na tukio la ujambazi uliotokea juzi katika mitaa ya Mlandege na Malindi na kuwajeruhi watu wawili akiwemo askari Polisi wa Kituo cha Malindi.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis Mkadam alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa 4:00 za usiku katika mitaa ya Magogoni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Kamanda Mkadam alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta watu wengine waliohusika na ujambazi huo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

“Jeshi letu tunaendelea kuwasaka watu wengine waliohusika na tukio lile huku kijana tuliemkamata akitusaidia kutuongoza kuwapata wenzake ili hatua za kisheria ziweze kuwabana ikiwemo kuwafikisha mahakamani,” alisema.


Akizungumzia kuhusu majeruhi waliojeruhiwa katika tukio hilo la ujambazi Kamanda Mkadam alisema Askari Polisi Sajenti Hija Hassan Hija anaendelea vizuri katika Hospitali kuu ya Mmnazimmoja huku Ndg.Salum Issa Suleiman amesafirishwa Tanzania bara, na jamaa zake kupata matibu ya jaraha lake.

Tukio hilo la ujambazi lilitokea Septemba 26 mwaka huu majira ya saa 8:30 mchana katika mitaa ya Mlandege na Malindi jirani na sheli ya Gapco, ambapo majambazi hao walifanikiwa kupora mfuko wa fedha unaosadikiwa kuwa na zaidi ya shilingi milioni 30.6m wa mfanyabiashara wa mchele nchini Salum Issa Suleiman (50) mkaazi wa Baghani ambapo alikuwa akizipeleka Benk ya Watu wa Zanzibar Tawi la Mlandege Mjini Unguja.

Katika tukio hilo Askari Polisi wa Kituo cha Malindi Sajenti Hija Hassan Hija alijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika sehemu ya mkononi na mguuni huku Mfanyabiashara Salum alijeruhiwa sehemu za miguuni.

1 comment:

  1. jina lake mbona hatulioni au munaogopa kwakuwa tutasema ndio faida za muungano? maana matokeo kama haya aghlab hufanywa na ndugu zetu wa damu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.