Habari za Punde

Wakulima wahimizwa kuitunza mikarafuu

Na Tatu Makame
 
MKUU wa kitengo cha  mazao ya biashara kutoka Idara ya Misitu na Maliasili  Zisizorejesheka, Is-haka Mohamed Abdulwakil, ametoa wito kwa wakulima wa karafuu kuwa na utamaduni wa kuitunza mikarafuu baada ya mavuno.

Wito huo aliutoa ofisini kwake Maruhubi,wakati akizungumza na mwanduishi wa habari hizi.

Alisema kumejitokeza mtindo wa baadhi ya wakulima kutokuwa na utamaduni wa kuitunza mikarafuu baada ya mavuno  na kusababisha mavuno ya karafuu kupungua msimu hadi msimu.

Alisema serekali inatumia gharama kubwa kuendeleza zao la karafuu, hivyo ni wajibu wa wakulima kuhakikisha wakati wote mikarafuu inakuwa safi.

Aidha aliwahimiza wakulima wapya wa mikarafuu kuomba kupatiwa miche ya mikarafuu ambayo hutolewa bure ili kuhakikisha kilimo cha mikarafuu kinarejea katika asili yake.

Alisema kutokana umuhimu wa zao hilo wameandaa  mafunzo maalum  yatakayowasaidia wakulima kujua namna ya kuitunza 
na kuihifadhi mikarafuu.


Nae Ofisa wa uzalishaji miche kutoka idara hiyo, Rashid Nasor Rashid, alisema mikakati yao  ni kuhakikisha kila mwaka wanazalisha miechi milioni moja na kuigawa kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.