Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.(WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI.)

Na.Mwashungi Tahir Maelezo.
Iko haja kubwa jamii kuwaheshimu wazee kwani bila ya wao kutulea kwa kutupa malezi mazuri kwa kutusomesha tusingelikuwa leo tuko hapa.
Hivyo iko haja kuwatunza , kuwalea na kuwathamini kwa malezi mema yao waliyotupa .

Hayo ameyasema mkuu wa Mkoa mjini magharibi Abdullah Mwinyi Khamis wakati alipokuwa akizungumza na wazee huko Dole wilaya ya magharibi katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani .

Amesema wazee wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii katika ujana wao katika kushiriki mambo mbali mbali ya kiuchumi  kiutamaduni  na vile vile kijamii katika serikali.

Hivyo tunahitaji kuwalea wazee kwa kuwatunza kwa kuwapa huduma  zikiwemo malazi kivazi  pia ikiwemo huduma ya kuwapatia chakula waweze kuwa na siha nzuri katika maisha yao.


“Serikali inatoa mchango mkubwa katika kuwaenzi wazee hao mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu mzee Karume aliwashughulikia kwakuwajengea nyumba za kuishi wazee hao pamoja na huduma nyengine zote za jamii” alisema Abdullah Mwinyi 

Abdullah Mwinyi ametoa wito kwa jamii iachane kuwatelekeza Wazee  na kutoa msisitizo kwa kuwahifadhi na kuwapa huduma nzuri kama ilivyo kwa kawaida kwa binaadamu.

Nae Katibu Mkuu wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii , Vijana , Wanawake na Watoto Asha Ali Abdullah amesema serikali imepitisha sera ya hifadhi jamii ya kulinda na kuwahifadhi wazee kwa vizuri.

Siku hii ni siku muhimu  inasherehekewa Duniani kote kila ifikapo tarehe 1-10-2014 ambapo ujumbe wa mwaka huu (WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI).

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Katibu mkuu Mufti shekh Soraga na M kuu wa Wilaya magharibi Ayoub Moh'd Mahmoud .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.