Habari za Punde

YOUTH FOR AFRICA (YOA) YATAMBULISHA TUZO ZA UNDER 30

PREES RELEASE
Introducing Under-30 Youth Awards and Call For Nominations
Youth For Africa (YOA), a National Youth led Organization based in Dar es Salaam wishes to inform the esteemed media and General Public about the Under-30 Youth Awards 2014, Tanzania’s First and Largest Youth Awards. Under the Theme “Beyond Norms”  Under-30 Youth Awards 2014 seeks to recognize Outstanding Under-30 Tanzanian Individuals and/or Groups so that they  get motivated to dream more, learn more and do more.
Youth For Africa (YOA) also wishes to inform the esteemed media and public that the Nominations for Young Generation between the ages of 18 to 30 years are now open to 15 Categories of the Under-30 Youth Awards 2014
Under 30 Youth Awards 2014 categories include agriculture, innovation, social impact, fashion designing, fashion modeling, music, film/drama, entrepreneurship, most appealing business idea, sports, broadcasting media, blogging, print media, fine art and academician.
 We also wish to acknowledge our proud sponsors namely Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), Uongozi Institute, Push mobile, Africa Media Group Ltd [channel10 & magic fm], FastJet , Onspot Magazine, Smartcodes ,Kalax Promotions and Adam Digicom . We call upon other stronger Partnerships and collaborations from Institutions, Government, Civil Society, Private Sector, Diplomatic Missions, Financial Institutions and the Public at large to achieve our Esteemed Goal.
The nomination period runs until 10 November 2014. Nomination can done via our SMS platform and Under 30 Youth Awards official website www.youthawards.or.tz
The SMS nomination (procedures)
Send the word (with no quotation) “ Under30 “ to 15678 and you will receive a message which shows all the categories and their corresponding codes. To complete nomination send the code name then put space/tab/enter and write the nominee name followed by the nominee contacts (phone no or email)

  


TAARIFA KWA UMMA
Kutambulisha Tuzo za Vijana chini ya Miaka 30 na kuanza upendekezaji majina ya vijana hao
Youth For Africa (YOA), Shirika la kitaifa  linaloongozwa na vijana  ambalo makao yake  yapo Dar es Salaam linapenda kuwataarifu wanahabari  na umma  kuhusu  tuzo za vijana chini ya miaka 30 kwa mwaka 2014 ( Under-30 youth Awards 2014). Tuzo hizi ni kubwa na za kwanza za aina yake zinazowalenga vijana moja kwa moja. Tuzo za mwaka huu zinakuja na ujumbe  ‘Zaidi ya Kawaida’ ikiwa ni katika kuwapa moyo na kuwahamasisha vijana kufanya vitu vizuri zaidi katika maendeleo yao binafsi, jamii na nchi kwa ujumla. Tuzo hizi za vijana wenye umri chini ya miaka 30 zinalenga kutambua  vijana wa kitanzania  walio chini ya miaka 30 ambao wamefanya vizuri katika nyanja mbalimbali na kuwatia hamasa wao na vijana wote wazidi kuwa na ndoto, wazidi kujifunza na wazidi kufanya vitu vizuri zaidi katika nchi.
Youth For Africa (YOA) pia inapenda kuwataarifu wanahabari  na umma kwa ujumla  kuwa upendekezaji wa majina ya vijana wanaostahili hizi tuzo (kuanzia miaka 18 hadi 29) ushafunguliwa  na unazingatia vipengele 15 vilivyopo tuzo hizi.
Vipengele hivyo  ni pamoja na Kilimo, Uvumbuzi, Mchango kwa Jamii, Ubunifu Mitindo, Uanamitindo, Muziki, Uigizaji, Ujasiriamali, Wazo zuri la Biashara, Michezo, Utangazaji, Tovuti bora, Uchapishaji, Sanaa, Uanataaluma..
Tunapenda kuwatambua na kuwashukuru wadhamini wetu waliojitokeza mpaka sasa ambao ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Uongozi Institute, Push mobile, Africa Media Group Ltd [Channel 10 & Magic fm], FastJet , Onspot Magazine, Smartcodes ,Kalax Promotions and Adam Digicom. Tunapenda kuchukua nafasi hii pia kuwakaribisha wadau mbalimbali waweze kudhamini tuzo hizi ili kuweza kutimiza malengo ya tuzo hizi.
Upendekezaji wa majina utaendelea mpaka tarehe 10 Novemba 2014. Mapendekezo yanatumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu au kupitia tovuti yetu. www.youthawards.com.
Kupitia ujumbe wa simu (maelezo jinsi ya kushiriki):
Tuma neno “ Under30 “ kwenda 15678 upate kujua vipengele vyote na code zake. Ukishakujua kodi za kila kipengele andika ujumbe mfupi wenye kodi ya kipengele unachotaka kupendekeza mtu ikifuatiwa na jina la mtu unayempendekeza na namba yake ya simu au barua pepe kasha utume kwenda 15678.
 
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Youth For Africa (YOA) Harisson Anthony Mbugi akihojiwa na mwandishi wa habari mudamfupi baada  ya kutambulisha rasmi tuzo za vijana chini ya miaka 30 na upendekezaji wa vijana hao, iliyofanyika Idara Maelezo jijini Dar es Salaam 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.