Habari za Punde

Ziara ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Pemba.

Mkuu wa Shirika la Bandari tawi la Shirika la Bandari Ndg Hamad Salim , wakati wa ziara ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Juma Duni akiwa katika ziara ya kutembelea Taasisi za Wizara yake kisiwani Pemba ikiwa mojaopo Shirika la Bandari Pemba kujitambulisha kwa Wafanyakazi wa shirika hilo.
Krini ya kupakulia mizigo, yenye uwezo wa tani tano, iliopo bandari ya Mkoani Pemba, ikiwa imeshaharibika kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, ambapo shirika la bandari Zanzibar linampango wa kunua nyengine yenye uwezo wa tani 40 wakati wowote. 
Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Pemba wakimsikiliza Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe Juma Duni, akiwahutubia wakati akiwa katika ziara ya kutembelea Wizara za Mawasiliano na Taasisi zake kisiwani Pemba katika ziara yake kujitambulisha kwa Wafanyakazi wake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba) 

2 comments:

  1. Pemba bandari bad kabisaa. Hebu name tumuombe huyo Bakhressa basi angalau atujengee mabanda ya kujistiri jua na mvua kama pale Malindi

    ReplyDelete
  2. Hilo tatizo ni lenu wenyenu kwani Rais ni kutoka Pemba, Makamo wa kwanza haisemeki, Waziri wa Miundombinu yenyewe ndio huyooo na huyo Bakhresa piaaaaaa sasa tatizo ni nyinyi wenyewe hamtaki kupeleka maendeleo kwenuuuu kwani nyooooote mnaondoka mnakuja huku sasa kule atatengenezewa naniiiiiiiii abaaaaaa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.