Habari za Punde

DK. SHEIN APELEKA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MFALME SALMAN ABUL-AZIZ AL- SAUD WA SAUDI ARABIA

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                             26 Januari, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amempelekea salamu za rambirambi mfalme Salman bin Abdul-Aziz Al-Saud wa Saudi Arabia kufuatia kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdulaziz Al Saud wa nchi hiyo kilichotokea hivi karibuni.
“Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar, natoa mkono wa pole kwako Mheshimiwa, kwa wanafamilia na wananchi wote wa Saudi Arabia” Dk. Shein amesema katika salamu hizo.
Katika salamu hizo Dk. Shein ameeleza kuwa dunia itamkumbuka sana marehemu Mfalme Abdullah bin Abdul-Aziz Al-Saud kutokana na uongozi wake wa busara, upendo wake kwa watu na dhamira yake katika kupigania amani, utulivu na maendeleo katika Mashariki ya Kati na duniani kote.
“Tunamuomba Mwenyezi Mungu amuweke marehemu Mfalme Abdullah bin Abdul-Aziz Al- Saud mahala mema peponi”alieleza Dk. Shein na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wanafamilia na wananchi wa Saudi Arabia kuwapa ustahamilivu na nguvu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.