Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi.

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.

WAZIRI wa n Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhamed Abuod Mohamed amesema atamuandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi kuongeza fedha za  usafiri kwa askari wa Jeshi la Polisi mara baada ya kustaafu na kurejea makwao.

Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wawakilishi Chukwani  wakati akijibu suali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma alietaka  kujua sababu za  askari pol;isi anapostaafu kulipwa shilingi 66,000 kwa ajili ya nauli yake na kusafirisha mizigo kwa masafa ya kilomita 20 kiwango ambacho ni kidogo na hakikidhi haja.

Waziri Aboud amesema  kutokana na kadhia  hiyo atalazimika kuandika barua kwa Waziri Nchimbi  kuliangalia suala hilo ili kulitafutia ufumbuzi na kuwaondoshea shida  asikari hao wanapostaafu.

Aidha Waziri huyo alisema kuwa Ofisi ya Makamu  wa Pili wa Rais Zanzibar  jukumu lake ni kuratibu masuala ya Muungano  na kazi ya usimamizi iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.`


Waziri Aboud  akitoa ufafanuzi wa madai  ya askari watatu waliostaafu kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo ilielezwa kuwa walipewa  milioni 16 ili kurudi  makwao kwamba taarifa hiyo sio kweli.

Alisema ana elewa kuwepo kwa askari hao na kusema askari anapostaafu hutaarishiwa usafiri wa mizigo pamoja na familia zao hadi makwao jambo ambalo hufanyika  kwa kutegemea mstaafu alikuwa na cheo gani.

Baada ya ufafanuzi huo alisema kuwa  Kamishna wa Polisi aliwaita askari hao ofisini kwake na kuwafahamisha utratibu ulivyo,na askari hao baadae  waliridhika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.