Habari za Punde

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja

Wanachama wa CCM wa Shehia ya Pete wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana akiwasali katika Tawi hilo la CCM, kupata taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi kwa Wananchi Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Kinana akisalimkiana na Viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati akiwasili katika Tawi la CCM Pete kupata Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM,kabla ya kuaza ziara yake katika Wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Kinana akizungumza na Watendaji na Viongozi wa CCM, baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kazi za kawaida katika Wilaya hiyo. 
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Abdulrahaman Kinana, akiwahutubia na kutowa maelekezo ya ufuatiliani wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika majimbo ya Wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Kinana, akishiriki katika ujenzi wa Taifa wa ujenzi wa Ofisi ya Jimbo la Mayuni,kitogani wakati akiwa katika ziara yake Wilaya ya Kusini Unguja.katika ujenzi huo Ndg. Kinana ameahidi kuchangia shilingi milioni mbili kukamilisha ujenzi huo.  

Msoma risala akisoma risala hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Omar Kinana, alipotembelea ujenzi huo na kushiriki ujenzi wa TaifaWenye miwani kushoto Mbunge wa Muyuni Mhe Mahadhi na Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe Jaku.   
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Kinana akimjulia hali aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Kusini Unguja Mzee. Haji Abdallah Mzee. akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Omar Kinana, akiwa na Viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kuzini Unguja akiende kuwatembelea Wakulima wa Mwani katika Kijiji cha Jambiani Kibigija
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Kinana, akisalimiana na Viongozi wa Kikundi cha Kilimo cha Mwani cha Nashukuru KwaHeri, alipowasili katika kijiji hicho akiwa katika ziara yake kutembelea miradi ya Wananchi na kuimarisha Chama.  
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana na Mwakilishi wa Muyuni Mhe. Jaku Hashim na Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM Kusini Unguja Ndg. Ramadhani Abdallah, wakielekea katika mashamba ya mwani baharini kuangalia shughuli za upandaji wa mwani. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Kinana akishiriki katika upandaji wa Mwani, katika moja ya mashamba ya mwani bahari akiwa na Mwakilishi wa Muyuni Mhe Jaku Hashim na Wakulima wa mwani jambiani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Kinana akishiriki katika upandaji wa Mwani, katika moja ya mashamba ya mwani bahari akiwa na Mwakilishi wa Muyuni Mhe Jaku Hashim na Wakulima wa mwani jambiani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akiondoa kipazia kuonesha ishara ya kuweka jiwe la msingi la ukumbi wa mkutano wa CCM Makunduzi, ukumbi huo unajengwa kwa nguvu za Mbunge na Mwakilishi na Wananchi wa Makunduchi.anayepiga makofi Mwakilishi wa Makunduchi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi huo Mhe. Haroun Ali Suleiman. 
Tangi jipya la Maji Safi na Salama likiwa katika ujenzi wake huko katika kijiji cha Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akimsikiliza Afisa wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Kusini Unguja Ndg. Hafidh Hassan, akitowa maelezo ya ujenzi wa Tanki jipya la maji safi na Salama kwa Wananchi wa Makunduchi, ambalo linaendelea na ujenzi wake. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.