Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abrahaman Kinana,akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Maziwa Fumba kilichojengwa na Muwekezaji Mzalendo wa Zanzibar Ndg Said Salim Bakressa , ikiwa ni miradi ya Wananchi kutoa ajira kwa Vijana.
Seheme ya uzalishaji wa maziwa katika kiwanda hicho kilioko maeneo ya Maeneo huru ya Uchumi Fumba Zanzibar eneo hili limetengwa kwa Wawekezaji wanaoekeza Zanzibar.
KATIBU Mkuu wa CCM Ndg.Abrahaman Kinana, akipata maelezo kutoka kwa Meneja
wa Kiwanda cha Maziwa cha Azam Ndg.Kirtikumar.Dave, wakati akiwa katika ziara
yake kutembelea miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Dimani jimbo la Dimani.
Sehemu ya Mziwa yanayozalishwa katika kiwanda hicho kwa ujazo tafauti,
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahamani Kinana akiwa na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Profesa David Mfininga, akipata maelezo ya
ujenzi wa Chuo Kikuu kilichoko Fumba Unguja wakati alipofika kuangalia
maendeleo ya ujenzi huo akiwa katika ziara yake Wilaya Dimani.
Profesa Nyandwi, akisoma risala ya uazilishi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Baharini kilichoko nje kidogo ya mjini wa Zanzibar katika maeneo ya Buyu, AKISOMA TAARIFA HIYO kwa Katibu Mkuu alipotembelea Chuo hicho kujionea ujenzi wake.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abrahaman Kinana akiwahutubia Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Baharini tawi la Zanzibar, akiwa katika ziara yake Zanzibar.
Wananchi wa Fuoni Kibondeni wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM alipofika kutembelea Kikundi cha Utunzaji wa Mazingira na kupanda mikoko katika eneo hilo la hifadhi ya mazingira.
Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Fuoni Kibondeni kilioko katika Jimbo la Fuoni, alipowasili katika kijiji hicho kupanda mikoko kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
Kiongozi wa Kikundi cha utunzaji wa Mazingira cha Fuoni Kibondeni akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana, kuelekea katika eneo la hifadhi ya mazingira kwa upandaji wa miti ya mikoko.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abrahaman Kinana akijumuika na
Wananchi wa Kikundi cha kuhifadhi Mazingira Fuoni kibondeni katika upandaji wa miti ya
mikoko ili kutunza mazingira ya eneo hilo , akiwa katika ziara yake kukagua
miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchanguzi kwa wananchi.
katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abrahaman Kinana
akilizindua Gari la kubebea Wagonjwa katika Jimbo la Fuoni lililotolewa na Mbunge na
Mwakilishi wa Jimbo hilo.uzinduzi huo umefanyika katika tawi la CCM Kijitoupele.
Na kuaahidi kuktowa mifuko 50 ya saruji ili kumalizia ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abrahaman Omar Kinana akizungumza na Wanachama wa CCM tawi la Kijitoupele Kwarara, akiwa katika ziara yake kutembelea miradi ya Maendeleo na kufuatilia Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Wananchi wake, na kuahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na shilingi milioni mbili kwa ajili ya umaliziaji wa Tawi hilo linalojengwa kwa Nguvu za Wananchi na Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Fuoni Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abrahaman Omar Kinana, akiwahutubia Wanamaskani Kaka ya Mtungujani Magogoni akiwa katika ziara yake kuimarisha Chama na kukagua ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015. na kutembelea miradi ya maendeleo katika majimbo ya Zanzibar. Na kuahidi fenecha baada ya ujenzi wake huo na kuwa kitega uchumi kwa Vijana kuwapa mtaji kuazisha biashara
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abrahaman Omar Kinana akiwa katika ujenzi wa Taifa katika ijenzi wa Maskani Kaka ya Mtungujani Magogoni Jimbo la Magogoni,akiwa katika ziara yake kutembelea Wilaya ya Dimani Kichama kuimarisha Chama na kufuatilia ahadi za CCM kutimiza Ilani ya Uchagunzi ya CCM kwa wananchi ilioitowa wakati wa kampeni ya uchanguzi 2010-2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa tawi la CCM Mwandapole ambalo lilitiwa moto na kuharibika kabisa kutoka na moto huo. Ndg. Ahmada Shaa, akisoma risala ya ujenzi wa Tawi hilo lililokuwa katika hatua kubwa ya ujenzi wake.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abrahaman Omar Kinana kushoto, akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ya Tawi la CCM Mwendapole Amani, Ndg. Ahmada Shaa na katikati Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndg. Yussuf Mohammed, wakiwa katika viwanja vya tawi hilo amani mwandapole Katibu wa CCM ameahidi kuchangia mabati 200 na saruji na mbao kwa ajili ya uwekezaji wake na kuitaka kumaliza ujenzi huo kabla ya sherehe za CCM zinazotarajiwa kufanyika mwezi wa Febuary2015
No comments:
Post a Comment