Mwanaharakati mkongwe wa maendeleo ya Makunduchi, ndugu Mohamed Simba akiwa na viongozi wa michezo katika maandalizi ya mbambano wa mpira wa miguu wa hisani baina ya magwiji wa kabumbu kutoka Italy na Zanzibar. Mpambano huo unaotegemewa kufanyika kwenye uwanja wa Amaan tarehe 7 Machi wakati wa usiku saa 2.00 unalengo la kukusanya fedha kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Kajengwa, Makunduchi. Kwa mujibu wa ndugu Simba maandalizi yote muhimu yameshafanywa.
Hii ni aina ya tiketi itakayotumika siku ya mpambano baina ya mastaa wa Italy na wale wa Zanzibar. Mechi hii imekuja kufuatia juhudi za ndugu Mbanja na ndugu Mohamed Simba katika kuipatia Kajengwa maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment