Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wakati akiingia kwenye uwanja wa
Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya
kuzaliwa kwa CCM ambapo kitaifa zimefanyika mkoa wa Ruvuma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na kijana wa chipukizi mara baada
ya kuwasili kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe za
maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Baadhi ya viongozi wakiwasili kwenye uwanja wa Maji Maji kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikwagua gwaride la chipukizi.
Vijana wa Chipukizi wakionyesha ukakamavu kwenye onyesho la Halaiki wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
Hivi ndivyo uwanja wa maji maji ulivyofurika kwenye sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 38 tangu kuzaliwa kwa CCM.
Vijana wa Chipukizi wakitoa heshima kwa mgeni rasmi.Vijana wa chipukizi wakionyesha ukomavu wao wa mafunzo wanayopata.
Vijana wa Chipukizi mbele ya mgeni rasmin Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yalioadhimishwa Mjini Songea leo.
Wananchi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 38 ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika Mkoani Songea leo, wakifuatilia sherehe hizo
Kepteni John Komba akiimba pamoja na Abdul Msimbano wakati TOT ilipokuwa ikitumbuiza wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Maji Maji na Kutambulisha nyimbo yao mpya.
Bendi ya TOT ikishambuliwa Jukwaa wakiwa chini ya Uongozi wa Kepteni John Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia hadhira iliyojaza watu kutoka kila kona ya mji wa Songea na majirani zake.
Vijana wakiangalia picha ya Hayati Abeid Aman Karume ,Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka 28 ya kuzaliwa CCM ambapo kitaifa zimefanyika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoa wa Ruvuma.
Msanii Diamond akiwaburudisha
maelfu ya watu waliofurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea
kwenye sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM ambazo kitaifa
zimeadhimishwa mkoani Ruvuma.
Mwananchi akiwa katika viwanja vya Majimaji Songea akifuatilia serehe za kutimia miaka 38 ya Chama cha Mapinduzi akichukua picha kupitia simu yake ya mkononi kiwanjani hapo.
Msanii wa Kizazi kipta Diamond akifanya vitu vyake wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya CCM katika viwanja vya mpira Majimaji Songea leo.(Picha na Adam Mzee)
He! hawa Wazanzibari vipi hakwenda mtu? hata raisi au wote washaingia cuf mana nasikia cuf imepata nguvu sana
ReplyDeleteama kweli wa ZNZ hiki si chama chenu
ReplyDeleteWazanzibar Hawajaalikwa wamefanya watanganyika tu , ndio huo ubaguzi tulokuwa hatuutaki , tuwacheni tupumue
ReplyDelete