Habari za Punde

OCD Kati ajeruhiwa kwa Ajali

Na Mwandishi wetu
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kati, Maulid Khamis, amelazwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja akitibiwa majeraha aliyopata baada ya kugongwa na gari katika eneo la Mtoni wilaya ya magharibi Unguja.

Kamanda huyo amelezwa eneo la Mapinduzi Kongwe katika hospitali hiyo baada ya kupata majeraha sehemu ya usoni na mguuni.

Kwa mujibu wa polisi, Kamanda Khamis, aligongwa na gari yenye namba za usajili Z 591BN iliyokuwa ikitokea Amani kuelekea Mtoni wakati Kamanda huyo akiendesha vespa yenye namba Z591DQ.

Dereva wa gari hiyo ambae alikimbia baada ya ajali, alimgonga kwa nyuma wakati akitokoea Amani kuelekea Mtoni.


Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari huku akishindwa kuchukua tahadhari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.