Mmoja wa wakunga wa jadi Bi. Namboto Sheha Kombo akielezea jinsi wanavyofanya kazi zao za ukunga katika mkutano uliofanyika Hospitali ya Kivunge Mkoa wa kaskazini "A" Unguja.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahamoud Thabit Kombo akizungumza na wakunga wa jadi, na kuwataka washirikiane na watalaam wa Afya katika kazi zao ili kupunguza vifo vya Akinamama na watoto.
Msaidizi daktari dhamana Hospitali ya Muembe ladu Ruzuna A.M. Shamte akifahamisha kitu katika mkutano wa wakunga wa jadi na watalam wa afya huko Kivunge Mkoa wa kaskazini "A" Unguja.Baadhi ya Wakunga wa Jadi na watalam wa Afya waliofika katika mkutano wa kukuza mashirikiano huko Kivunge Mkoa wa kaskazini "A" Unguja wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahamoud Thabit Kombo (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
Dkt. Dhamana Hospitali ya Kivunge Khamis Hamad Ali akitoa nasaha zake katika mkutano wa Wakunga wa Jadi na watalam wa Afya wa kukuza mashirikiano katika kufanya kazi zao. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment