Habari za Punde

Kwa nini nyuki wa kaskazini Unguja wagoma kutengeneza asali?

Picha ya pamoja ya Wafugaji wa nyuki wa Unguja baada ya majadiliano  mazito na swali lililochukuwa muda wao mrefu ni kupungua kwa uzalishaji wa asali kutoka kaskazini Unguja kutokana na nyuki wa huko kugoma kutengeneza asali katika maeneo mengi ya huko.
 
Majadiliano hayo yaliyofanyika afisini kwa wafugaji nyuki hapo Maruhubi yalihudhuriwa na wafugaji kutoka Kusini na Kaskazini ya Unguja.
 
Mfugaji mkongwe kutoka Sundsvall, Sweden bibi Christin amependekeza kujaribu kuchukuwa "malkia" kutoka Kusini Unguja na kuwapeleka Kaskazini.
 
Bi Christin ambaye ni mratibu wa mashirikiano kati ya Manispaa ya Sundsvall na wadi za Makunduchi anayo nia ya kuanzisha ufugaji nyuki Makunduchi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.