TAARIFA YA TAHADHARI KWA WANANCHI NA VYOMBO VYA
HABARI JUU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KATIKA
KIPINDI CHA MVUA ZA MASIKA
Ndugu wananchi na wafanya biashara,
kama mnavyojua kuwa hivi sasa
tunakabiliwa na kipindi cha mvua za masika zinazotarajiwa kunyesha hivi
karibuni ambapo mvua hizo zinatarajiwa kuwa kubwa kwa mujibu wa taarifa za zinazotolewa na
wataalamu wa mamlaka ya hali ya hewa tanzania kanda ya zanzibar.
Kutokana
na uzoefu wa mvua za masika maranyingi mji wetu huathiriwa na mafuriko katika
mitaa na kusababisha athari kubwa kwa jamii kama vile maradhi ya
mripuko(kipindupindu,matumbo ya kuharisha na kuharisha damu,homa ya
dengue,uharibifu wa makaazi , upotevu wa mali na hata kusababisha vifo kwa
wananchi.
Hivi sasa baadhi ya wananchi wanatabia ya ya
kuchafua mazingira na kuhatarisha afya za wakaazi kwa kufanya mambo yafuatayo
kinyume na utaratibu na sheria nayo ni:
·
utupaji
taka ovyo katika maeneo ya makaazi,magofu,maeneo ya wazi na ndani ya michirizi
na mitaro ya maji ya mvua.
·
uuzaji
holela wa biashara za matunda na vyakula kama vile juisi ya maji ya
muwa,mamalishe,urojo,chipsi na samaki wa kukaanga katika maeneo machafu na
yasiyoruhusiwa kisheria na kutofuata kanuni za afya.
·
kutiririsha
maji machafu ovyo mitaani ambayo husababishwa na ukosefu na kujaa kwa makaro.
·
ukosefu
wa vyoo na kufanya haja kubwa ovyo .
·
kuwa
na makaazi yaliyozungukwa na majani marefu.
Kwa
taarifa hii baraza la manispaa linawaomba wananchi,viongozi wa shehia na
wadi,wafanyabiashara,vikundi vya mazingira na wadau mbali kufanya mambo
yafuatayo:
·
kusafisha
mazingira yanayokuzunguka kwa kuondoa taka na kufyeka majani marefu mitaani.
·
kuzuia
umwagaji wa maji machafu ovyo mitaani na kusafisha michirizi ya maji ya mvua
·
kufukia
vidimbwi vyote vya maji ili kudhibiti
mazalio ya mbu nk.
·
kutupa
taka katika maeneo ya majaa maalum yaliotengwa na manispaa kwa ajili ya
kuhifadhia taka hizo.
·
kuzuia
uuzaji wa vyakula katika mazingira machafu na yasiyoruhusiwa kisheria kama vile
juisi ya maji ya miwa, mama lishe, urojo, chipsi nakadhalika.
·
kusafisha
maeneo yote ya magereji ya magari na magofu yaliotupwa taka kinyume na sheria.
·
kuacha
tabia ya kutupa taka katika mitaro na michirizi ya maji ya mvua.
·
kutouza
biashara za vyakula wazi na kutopanga biashara chini hasa katika maeneo ya
masoko.
·
kuandaa
utaratibu wa kusafisha mitaa kwa mashirikiano na vikundi vya usafi vya shehia
na wadi.
Katika
kukabiliana na changamoto zilizotajwa baraza la manispaa Zanzibar limepanga
mikakati ya kuimarisha usafi wa mazingira kwa kushirikisha wafanyakazi
wake,vikundi vya usafi,viongozi wa shehia na wadi na wadau mbalimbali kufanya
yafuatayo.
·
kusafisha
na kuweka makontena katika vituo vya taka kwa utaratibu maalum.
·
kuimarisha
timu ya ukaguzi wa afya na mazingira katika mitaa,maeneo ya biashara na masoko
ili kuhakisha kuwa mashart,kanuni na sheria za usafi zinatekelezwa
·
kuhamasisha
viongozi wa mitaa madiwani na masheha kuandaa mpango wa usafi katika shehia na
kuelimisha jamii juu ya matumizi mazuri makontena ya taka yanayotarajiwa
kuwekwa hivi karibun.
·
kusfisha
mitaro ya maji ya mvua kwa kushirikisha vikundi vya kijamii kwa kujitolea na
kulinda uhalibifu usitokee.
·
kutoa
elimu ya usafi na mazingira kupitia vyombo vya habari,mikutano ya jamii
mitaani.
·
kuendeleza
zoezi la operesheni maalumu ya kuzoa na kuondosha taka majaani
·
kutanua huduma za usafi katika maeneo
yasiyokua na huduma hiyo.
Ili
kufanikisha adhima hii baraza la manispaa linawaomba
wananchi,wafanyabiashara,viongozi wa mitaa,vikundi vya usafi,kamati za afya na
mazingira na wadau mbali mbali kusimamia kikamilifu mpango huu ili kuimamarisha
usafi wa mazinira na afya za wananchi na wageni wanaotembelea nchi yetu.
“kinga ni bora kuliko
tiba”
No comments:
Post a Comment