Habari za Punde

Uzinduzi wa Hospitali Mpya ya Kisasa Iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk. Shein Vuga leo.

 

Jengo la Hospitali ya ilijulikanayo ya jina la Tasakhtaa inayomilikiwa na Mfanya Biashara Maaruf Zanzibar Salim Turkey iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Muekezaji Mzalendo wa Hospitali ya Tasakhtaa Mhe.Salim Hassan Turky, akimpokea Rais wakati akiwasili katika viwanja vya Hospitali hiyo kwa ajili ya uzinduzi wake uliofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mfanyabiashgara maarufu Ndg AbdulZakaria.katikati ni mmiliki wa hospitali hiyo Mhe Salim Turky 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa Global Hospital Dk K. Ravindranath,wakati alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa hospitali hiyo ya kisasa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi wa VIGOR Ndg Tofik Turky

Mhe Salim Turky akiwatambulia Viongozi wa Hospitali ya Tasakhtaa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya hospitali hiyo vuga kwa ufunguzi wake leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akivungua kipazia kuashiria kuifungua Hospitali mpya na ya Kisasa ya Tasakhtaa, uzinduzi huo umefanyika leo kushoto Mmiliki wa hospitali hiyo Mhe Salim Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Hospital ya Kisasa ya Tasakhtaa, kulia Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa Global Hospital Dk. K.Ravindranath na kulia Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe Salim Turky 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkuu wa Chumba cha Maabara Dk. Saghir Ahmad, wakati akitembelea hospitali hiyo baada ya kuifungua rasmin leo asubuhi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Daktari Mkuu wa Hospitali ya Tasakhtaa Dk Nagesh.K. alipotembelea chumba cha Cityscan katika hopitali hiyo akipata maelezo ya mashine hiyo ya kisasa itatowa huduma kwa wananchi watakaofika kupata huduma hiyo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mhe Salim Turky akitowa maelezo ya matumizi ya CityScan hiyo mpya na ya kisasa.

        Mashine mpya na ya Kisasa ya City Scan ikiwa katika hospitali hiyo mpya ya kisasa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo akiwa katika Chumba maalum cha huduma ya wazazi wakati akitembelea jengo hilo la hospital hiyo baada ya kuifungua rasmin leo. mjini Zanzibar mitaa ya vuga. 
        Mashine za kuhifadhi watoto wachanga waliokuwa bado kutimia miezi tisa kikiwa katika hiyo.
Dk. K.Ravindranath, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipotembelea baadhi ya vyumba vya huduma kwa wazazi katika hospitali hiyo akiwa katika chumba maalum cha kuzalia kina mama katika hospitali hiyo.

                       Chumba cha Widi ya ICU katika hospitali hiyo ya Tasakhtaa Vuga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya matumizi ya mashine ya kisasa ya X-Ray kutoka kwa Dk K.Ravindranath.
                        Chumba cha Mashine ya Digitali ya X-Ray katika hospitali hiyo

Mtaalamu wa chumba cha uporesheni katika hospital hiyo Dk Sridhaar, akitowa maelezo ya mashine ya Digital ya kufanya uchunguza wa maradhi ya tumbo kwa kutumia mashine hiyo bila ya kufanyiwa uporesheni ya kupasulia hutumika mashine hiyo kutibumaradhi yao, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo la hospitali hiyo leo baada ya kuifungua rasmin kutowa huduma ya Tiba kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania.akiwa na mmiliki wa hospitali hiyo Mhe Salim Turky.(Mr White)
Mhe Turky akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika moja vyumba wa hospitali hiyo wakati ufunguzi wake.
Ust Jamal Murtadha akisoma Quran wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo jipya la hospitali ya Tasakhtaa Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na viongozi meza kuu wakimsikiliza msoma Quran wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza msoma Quran Ust. Jamal Murtadha akisoma wakati wa hafla hiyo.

Mmiliki wa Hospitali ya Tasakhtaa Zanzibar Mhe Salim Turky akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutowa maelezo ya mafanikio ya ujenzi wa Hospitali hiyo, kwa Rais wa Zanzibar na Wananchi waliohudhuria sherehe hiyo ya uzinguzi wake rasmin uliofanyika leo 28-3-2015.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Waziri wa Nchi Ofisi ra Rais Ikulu Mhe Dk Mwinyihaji Makame na Dk K Ravindranath wakimsikiliza Mhe Salim Turky akizungumza wakati wa hafla hiyo. ya uzinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hospitali ya Tasakhtaa Zanzibar, akitowa nasaha zake kwa muwekezaji huyu,
Baadhi ya wageni Waalikwa kutoka Comoro wakifuatilia na kumsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia hafla hiyo.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya Uzinduzi wa Hospitali mpya na ya kisasa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar.
Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi zao Zanzibar wakifuatilia hala hiyo wakati Rais wa Zanzibar akihutubia hafla hiyo.


            Mkurugenzi wa ZIPA Ndg Salum Khamis Nossor akizungumza wakati wa hafla hiyo

           Baadhi ya Waalikwa wakiwa katika ukumbi wa sherehe wakifuatilia hafla hiyo ya ufunguzi.
                         Wafanyakazi wa Makampuni ya VIGOR wakifuatilia hafla hiyo
               Mwakilishi wa Familia ya Turky akitowa neno la Shukrani baada ya hafla hiyo
Shekh Ahmeid Alawi kutoka Comora akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla ya sherehe za uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya Tasakhtaa Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu wakisitikia dua ya ufungaji wa sherehe hizo iliosomwa na Shekh kutoka Visiwa vya Comoro Shekh Ahmeid Alawi.
               Baadhi ya Wananchi waliohudhuria ufunguzi wa hospitali ya Tasakhtaa wakiitikia dua.



5 comments:

  1. hapo wafanya biashara lazima tukupongezeni, mumefikiria kitu cha maana sana kiasi kwamba hata hiyo serikali yetu hawajawahi kufikiria kitu kama hichi, tutapumzika kwenda bara kufuata matibabu, lakini tu malengo yawe ni kusaidia watu sio kukomowa watu, Allah akuzidishieni kheri muzidi kutusaidia

    ReplyDelete
  2. Mimi naomba taaluma kidogo hivi hiki kifaa kinaitwa city scan (kama kilivyoandikwa hapo juu) au ni C. T. Scan?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Computerized Tomography (CT scan)

      Delete
  3. Tungewaomba wanaohusika na hii hospitali mpya wasitumie kitega uchumi chao kwa kuwawezesha wenye nafasi za fedha kufaidika peke yao,bali pawekwe mfumo wa upatikanaji wa matibabu hata kwa wale wenye hali dhaifu.Ziko hospitali nyingi duniani zenye utaratibu kama huo,kwa mfano hospitali zilizoanzishwa na mchezaji mashhuri wa cricket huko Pakistan,yaani Imran Khan.



    kwa wale wenye hali dhaifu.Kuna mifano minhi

    ReplyDelete
  4. kama itakuwa malipo yake nafuu na huduma nzuri basi hatutowanufaisha tena watanganyika, maana maana mpaka panadol wakikuandikia basi wanaandika wanavyojuwa wao ili usifahamu kimeandikwa nini ili hata dawa ununuwe hapo hapo wakubamize

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.