Habari za Punde

Wajumbe wa Bunge la Norway watembelea Pemba

 MENEJA wa shirika la Umeme Zanzibar ZECO, Hassan Ali Mbarouk akiwaeleza jambo kuhusu mashine za kuzalishia umeme zilizopo Wesha Chake Chake , wajumbe wa bunge la Norway wakati walipokuwa kisiwani Pemba kuangalia matumizi ya fedha walizozitoa kwenye mradi wa umeme wa Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 KIONGOZI wa msafari wa wabunge wa Bunge la Norway Bw: Geir Hermansen akizungumza na wananchi wa Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba alipofika kwenye soko la kijiji hicho kuangalia maendeleo na matumizi ya nishati ya umeme, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 MBUNGE wa jimbo la Akershus nchini Norway   Mhe Abid Rada akisakata msewe uliopigwa na kikundi cha Kambini Kichokochwe ili kuwaburudisha wabunge hao walipofika kijiji cha Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba ili kuangalia matumizi ya umeme ulivyosaidia maendeleo ya wananchi, (Picha na Haji Nassor, Pemba).  

WABUNGE kutoka Norway wakiangalia bidhaa ya inayotengenezwa kwa mnazi wakati walipofika Konde wilaa ya Micheweni Pemba kuangalia matumizi ya umeme kutoka Tanga- Pemba unavyosaidia kuimarisha maisha ya wananchi, (picha na Haji Nassor, Pemba).  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.