Habari za Punde

Balozi Seif Akabidhi Msaada wa Vifaa kwa Wananchi wa Matemwe.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vipaza sauti Amiri  wa Jumuiya ya Sherehe za Siku Kuu ya Iddi Matemwe Ustaadhi Kundi Choum Haji kutekeleza ahadi aliyoip[a Jumuiya hiyo wakati wa sherehe za siku kuu ya Iddi el Hajj iliyopita.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman  Iddi akimkabidhi  mchango wa Shilingi 400,000/-  kwa kila kikundi miongoni mwa  vikundi 14 vya Ushirika wa Akina Mama vilivyomo ndani ya  Wilaya ya Kaskazini “ A “.
Balozi Seif akikabidhi Seti moja ya Jezi na Mipira kwa kila Timu ya Soka miongoni mwa timu nne zilizomo ndani ya Jimbo la Matemwe.
Balozi Seif akiangalia hodhi linalojengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji kwenye Msikiti Mkuu wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni kufanya Tathmini ya uenzi wa Vyoo ili uwahi kufunguliwa katika muda muwafaka uliopangwa.(Picha na – OPMR).

1 comment:

  1. Assalaam alaykum
    Huyu balozi sefu na no zwarde wanajifanya wakarimu sana kwa kutowa misaada lakinii la kujiuliza hizo pesa anazitowa wapi na vile vile anapokuwa kwenye viriri vya siasa anadiriki kuwa kadhifu madhekhe wetu eti wako huko wanaunya kwrnye ndoo.Balozi Sefu fahamu yakuwa cheo au ungozi ni dhamana na utakuja kuulizwa siku ya siku ambayo sisi sote tutakusanya na kuhukumiwa kwa matendo yetu ya duniani.Pumzi zinatudanganya na kujisahau kutokana na kauli zetu na vitendo vyetu.Tuikumbuke siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipoluwa cha Allaah pekee na jee tumejiandaa vipi?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.