Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Ndg Borafya Simali akizungumza wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani Kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini Unguja, iliofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar jumla ya shilingi milioni 400, zimechangiwa usiku huo, Fedha taslim shilingi milioni 91.2 zimechangwa usiku huo na ahadi iliotolewa ni shilingi milioni 316.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, na Viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Salama wakifuatilia hafla hiyo ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini Unguja. anaefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Shamsi Vuai Nahodha.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Viongozi wa Siasa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya kuchangia Mkoa wa Mjini iliofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Mhe Edward Lowasa akisalimiana na Mhe Steven Wasira wakati alipowasili katika ukumbi wa Salama Bwawani kuhudhuria Harambee ya Kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Mkoa wa Mjini Unguja wakati wa chakula cha hisani.kilichoandaliwa kwa ajili ya hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi picha ya Mzee Abeid Amani Karume Mfanyabiashara Tofiq Salim Turky baada ya kuinunua katika mnada huo iliuzwa shilingi milioni 5, ikiwa ni kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Mkoa wa Mjini Unguja Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Picha ya Kuchanganya mchanga kuashiria kuunganisha Zanzibar na Tanganyika na kupatikana Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Baada ya kubarikia picha hiyo Mtoto wa Mzee Nyerere Ndg Makongoro Nyerere aliyoinunua kwa shilingi milioni 2.5, katika mnada huo wa kuchangia mfuko wa maendeleo.
Baadhi ya washiriki wa Chakula cha Hisani Kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini Unguja wakifuatilia hafla hiyo iliofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, akiangali moja ya picha iliopingwa mnada ikimuonesha wakati wa kuapishwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akikaguwa bwaride rasmin katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Picha Mhe Mohammed Raza baada ya kuinunua katika mnada huo kwa shilingi milioni 5,
Baadhi ya Viongozi wa Serekali na Wafanyabiashara wakifuatilia hafla hiyo ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Wananchi na Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiwa katika ukumbi wa Salama Bwawani wakifuatilia hafla ya kuchangia mfuko wa Maendeleo ya Mkoa wa Mijini Unguja Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Picha ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akikagua bwaride la kwanza kwake baada ya kuapisha katika viwanja vya Uwanja wa Taifa Dar-es-Salaam, baada ya kununuliwa na Mstahiki Meya Dk Didas John Massaburi, baada ya kuinunua katika mnada huo kwa dola 1000.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi picha ya Marais wa Zanzibar kwa Awamu Tafauti, ilionadiwa katika Mnada huo wa kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Mkoa wa Mjini Unguja, akipokea picha hiyo Mhe Wakili R.G.Ishengoma, aliinunua kwa shilingi milioni 3. wakati wa mnada huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mhamed Shein, akimkabidhi Kitabu cha Miaka 50 ya Muungano ambacho kilipingwa mnada na kununuliwa na Mhe Haji Omary Kheri kwa shilingi milioni 15.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika ukumbi wa Salama wakifuatilia hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein, akipokea mfano wa cheki ya shilingi milioni mbili kutoka kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Zanzibar Gallery
Ndg Javed Jaffar kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein, akipokea mfano wa cheki ya shilingi milioni mbili kutoka kwa
Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Pietro Fiorentini Ndg Abdulsamad Abdulrahim, kwa ajili ya
kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini na kutowa Skolashipi 3 kwa Vijana
kwenda Uingereza kusomema Utafiti wa Mafuta.
Baadhi ya Wafanyabiashara wakishiriki katika hafla ya Chakula cha Hisani Kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini Unguja, Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti cha kushiriki katika kuchangia Mfuko
wa Maendeleo ya Mkoa wa Mjini Unguja, Ndg. Abass Ali Hassan Mwinyi akipokea Cheti hicho
kwa niaba ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa mchango wake katika kuchangia Mfuko huo.
Dk Shein Mgeni Rasmin Katika Chakula cha Hisani Kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Mjini Unguja Zanzibar. mbona naona kama ipo kichama au ???????, sawa hayo maendeleo tu tuyaone na ingekuwa vizuri tungeambiwa huo mchango utatumika kwa kufanyiwa nini
ReplyDeleteThen nimpe kura yangu ya ndio Maalim Seif Sharif , kesho kwa Allah ntaenda kujibu nini?
ReplyDelete