Habari za Punde

Maalim Seif aweka mawe ya msingi matawi ya CUF kaskazini Unguja

 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika barza ya CUF ya WENYE WIVU WAJINYONGE katika eneo la Kitope Mkaratini.
Vijana wa barza ya HATUDANGANYIKI  ya Kiwengwa Cairo wakimsikiliza Maalim Seif wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika barza hiyo (Picha na OMKR)

Na Hassan Hamad, OMKR

 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameweka mawe ya msingi na kupandisha bendera katika matawi na barza sita za CUF ndani ya Jimbo Kitope Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja. 
 
Matawi na barza alizoweka mawe ya msingi ni pamoja na Kiombamvua, Mkaratini, Mgambo, Kilombero, Kipandoni na Kiwengwa Cairo. 

Hata hivyo, mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike katika viwanja vya Kipandoni umehairishwa, kwa madai kuwa haukupata kibali kutoka kwa jeshi la polisi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.