Habari za Punde

Matukio Zenj Mitaani

 Msongamano wa magari barabarani husababishwa na maderevya wasio makini kutokana na kubishana wakiwa barabarani kama wanavyoonekana maderevya hawa wakibishana katika makutano ya barabara ya biziredi na muembeladu na kusababisha msongamano wa magari kwa muda wa nusu saa 
Wanafunzi wa Skuli mbalimbali Zanzibar wakiwa katika kituo cha daladala wakisubiri usafiri wa kurudi nyumba baada ya masomo yao. Kuna baadhi ya daladala huwakatalia kuwachukua katika gari zao kwa sababi ya nauli yao ndogo na kuchukuwa wananchi wanaolipa fedha kamili na kutumia muda wao mwingi vituo kusubiri usafiri kama wanavyoonekana wanafunzi hao wakiwa katika kituo cha kijangwani wakisubiri usafiri huo. wakati wa jioni

1 comment:

  1. Niliwahi ku-comment kuhusu hili la watoto Wa shule na usafiri Wa daladala na adha kubwa wanayoipata wanafunzi katika usafiri. Sijui Sheikh Maulid unatusaidia vipi kuufikisha maoni yetu pamoja na ujumbe ambao wewe mwenyewe unatuekea kwa wahusika. Ni jukumu la waandishi kufichua kero mbalimbali za wananchi na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi. Kuna tabia nyengine mbaya imezuka siku hizi , madereva wengi wa daladala hasa Wa Fuoni zinapokaribia nyakati za jioni hawafiki mwisho Wa kituo. Wengi wao hufika melitano msikitini. Huu ni ukiukwaji mkubwa Wa haki za abiria. Tunakuomba ndugu muandishi Fanya juhudi zako binafsi kutusaidia sisi wanyonge ambao usafiri Wa daladala ni sehemu ya maisha yetu ya kula siku.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.