Habari za Punde

Semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Andymicheel Grimany akifungua semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya chakula na Dawa iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Afisa Mipango  Idara ya Sera na Utafiti katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi Omara Ali Omar akitoa mada ya Usalama wa chakula katika uzalishaji kwa upande wa Mifugo katika Semina ya  siku moja ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya chakula na Dawa Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani.
 Mshiriki wa semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula  iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Saleh Mohd Haji akitoa amchango wake.
 Mrajisi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othman Simai akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala yaliyoulizwa katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni, (kulia) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Grimany. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

 Mkuu wa Idara ya Huduma za Maabara Bodi ya chakula, Dawa na Vipodozi Nadir Khamis Hassan akitoa mada katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.

 Meneja wa Kiwanda cha Maziwa cha Azam Zanzibar Kirtikumar Dave akichangia katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula wakifuatilia mada zilizowakilishwa kwenye semina hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.