Habari za Punde

Ukosefu wa usalama wa chakula ndio chanzo cha maradhi mengi

Na Fatma Kassim

MWAKILISHI wa Shirika la afya ulimwenguni WHO Zanzibar Dk Andymicheel Grimany amesema kuwa maradhi mengi yanayotokea kwa binaadamu chanzo chake ni ukosefu wa  usalama wa chakula.

Amesema kuwa kunaumuhimu wa kuzingatia uimarishaji wa chakula tokea kikiwa shambani uhifadhi wake hadi kufikia walengwa hakizingatii ubora na usalama wa chakula.

Hayo ameyaeeleza katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya Afya Duniani uliowakusanyisha wadau mbali mbali katika uliofanyika katika Zanzibar Beach Resort ambapo ujumbe wa mwaka huu ni ubora wa usalama wa chakula.

Alisema kuwa chanzo kikubwa cha maradhi yanayotokana na chakula ni pamoja na Ebola iliyotokea katika nchi za Afrika Magharibi pamoja na miripuko ya maradhi mabali mbali yanayotokea hapa nchini ikiwemo maradhi ya kuharisha.

Alifahamisha kuwa hivi sasa ulimwenguni kote kunaongozeko kubwa la matatizo  yanayotokana na ukosefu wa ungalizi mzuri wa vyakula vinayotokana na kilimo, Mifugo na hata katika utaarishaji wake na kusababisha maradhi kwa watumiaji.

Kwa upande wa Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa ni vyema wafanyabiashara hapa nchini kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kupunguza ongezeko la matatizo ya kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

Alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uekezaji wa bidhaa ya mifugo zikiwemo minofu ya kuku ambao baadhi yao hawafati taratibu za uuzaji kwa kuwahifadhi kwenye mafriji na badala yake baadhi yao husambaza kwa kutumia baskeli jambo ambalo linahatarisha afya za wananchi


Alifahamisha kuwa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi itaendelea kufanya uchunguzi pamoja na kudhibiti bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu sambamba na kuzitaka taasisi zote pamoja na wananchi nchini kujenga ushirikiano kwa lengo la kudhibiti bidhaa zisizofaa.

Wakitoa mada wakufunzi mbali mbali wa mkutano huo walisema kuwa kunachangamoto mbali mbali zinaikabili Bodi hiyo ikiwemo Zanzibar kugeuzwa jaa la bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu, ongezeko wa ghala zisizosajiliwa pamoja na uelewa mdogo wa jamii juu ya kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.

Walisema ni jukumu la wafanyabiashara wa chakula kujua sheria mbali mbali zinazosimamia masuala ya chakula sambamba na kutambua kuwa jukumu la usalama wa chakula ni lao.
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi ni chombo halali kilicho chini ya Wizara ya Afya na kina mamlaka ya udhibiti wa ubora wa usalama wa Chakula Dawa na Vipodozi pamoja na vifaa Tiba.
Tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 2007 zaidi ya tani 1000 zimeangamizwa          na zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa ya chakula hutegemewa kutoka nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.