Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mama Asha Balozi Seif, wakiwatembelea Wananchi waliohifadhiwa katika Kambi
maalum iliofunguliwa katika Skuli ya Mwanakwerekwe Unguja wakipata maelezo
kutoka kwa Mkuu wa Kambi hiyo Afisa Mdhamini wa Idara hya Maafa Zanzibar Bi
Hamida Mussa.
WAananchi waliopata maafa wakiwa katika kambi maalumu
iliotengwa kwa ajili yao, katika skuli ya sekondari ya mwanakwerekwe C,kuishi kwa muda katika kambi hiyo,
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wananchi wanaoishi katika kambi ya
Mwanakwerekwe Unguja baada ya nyumba zao kujaa maji kutokana na Mvua. Kulia Mke
wa Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif na kushoto Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk Khalid Salum.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk
Khalib Salum, akitowa maelezo ya kambi hiyo ya Wanaoishi Wananchi waliopata
Maafa ya Mvua za Masika zilizonyesha hivi karibuni na kuleta madhara kwa
familia mbalimbali kukosa pa kukaa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Abdallah Mwinyi Khamis, akizungumza wakati wa ziara ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuwatembelea na kuwafariji na kutowa misaada ya Kijamii kwa Wananchi hao.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akizungumza na kuwafariji Wananchi waliopata Maafa ya Mvua wakati wa ziara ya Mama Mwanamwema Shein, na Ujumbe wake wa Wake wa Viongozi wa CCM Wabunge na Wawakilishi.
Wananchi waliopata maafa wakiwa katika kambi maalumu iliotengwa kwa ajili yao katika Skuli ya Sekondari ya NMwanakwerekwe C, Zanzibar ,wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akipofika kuwafariji na kutowa misaada kwa ajili yao.
Mmoja wa Mwananchi wa Kwahani Bi Manaharusi Mwinyi, akitowa shukrani kwa niaba ya
Wananchi waliopata maafa wanaoishi katika kambi hiyo akitowa shukrani kwa Mke
wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake wa Wake wa Viongozi wa Wawakilishi na Wabunge waliofika katika
kambi hiyo kuwafariji kwa maafa hayo.
Mmoja wa Wananchi waliopata mafaa ya Mvua za Masika zilizonyesha hivi karibuni katika maeneo ya Zanzibar akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,
akimfariji na kumpa mkono wa pole Ndg. Suleiman Ramadhani, kwa kufiwa na ndugu yake Haji Habibu, wakati wa maafa ya mvua za masika.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema
Shein, akimkabidhi kiti maalum (wheel chair) Bi. Fathiya Rashid, kwa ajili ya
mzee wake Bi Safia Omar ni mmoja wa mwananchi alieathirika na mvua katika maeneo
ya kwahani Unguja.kushoto Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Mhe Ayuob Mohammed
Mahmoud.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Kanga Afisa Muandamizi Idara ya Maafa na Mkuu wa Kituo cha
Waathirika wa Mvua Bi Hamida Mussa. Kwa ajili ya Wananchi wa kituo hicho.
No comments:
Post a Comment