Maisha Lab ya
Uganda wametangaza kuwa warsha yao nyingine itafanyika Zanzibar wakati wa ZIFF
2015 mwezi Julai kuanzia tarehe 18 hadi 25. Maombi toka kwa wanaotaka kushiriki
katika warsha hii yameanza kupokewa na mwisho wa maombi ni tarehe 13 Juni.
Warsha za Maisha
Lab zimekuza vipaji vya waandishi wa filamu na wakurugenzi wa filamu wengi hapa
Afrika Mashariki. Tayari warsha hizo zimefundisha zaidi ya watu 1000 tangu
Maisha Lab ianzishwe.
Mkurugenzi wa
Maisha Lab aliyeko Kampala Uganda alisema kuwa wanataraji kutoa skolaship 60
kwa wanafunzi kwa mwaka kwa washiriki toka nchi zote za Afrika Mashariki.
“Katika warsha
zetu watu 60 (15 toka kila nchi) watachaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo
yatakayoongozwa na wakufunzi waliobobea katika fani za uandishi wa filamu. Nia
ni kuongeza ujuzi na kupanuwa wigo wa
biashara ya utengenezaji filamu hapa Afrika Mashariki.” Alisema Fibby Kioria
Mkurugenzi wa Maisha lab.
Katika kila
Warsha script zitashindanishwa na mshindi atapatiwa $5000 ili kumwezesha
kutengeneza filamu fupi katika mwaka unaofuata. Mwaka jana Nassir Qassim wa
Tanzania ndiye aliyeibuka mshindi.
Hii ni warsha ya
3 itakayofanyika Zanzibar na ZIFF ndio mdhamini wake ili kuwapa washiriki
nafasi ya kushiriki katika tamasha na hivyo kuweza kukutana na watengeneza
filamu wengine toka nje wanaokuja kwa ZIFF. Pia wanapata nafasi ya kuangalia
filamu tele zinazoonyeshwa wakati wa Tamasha.
Lakini
Mkurugenzi wa ZIFF aliharakisha kusema kuwa anasikitishwa sana kuona kuwa
washiriki toka Zanzibar huwa wachache kila mwaka. “Tunajuwa kuwa waandishi wa
filamu toka zanzibar wanahitaji sana mafunzo haya maana yanawapa ujuzi na pia
nafasi ya kujuana na watengeneza filamu wengine wa kimataifa”, alisema
Mkurugenzi huyo
Tasnia ya filamu
ya Bongo Movies imesemwa sana kwa kuwa na hadithi dhaifu kimataifa. Kwa kutumia
warsha kama hizi wadau wanaweza kukuza vipaji vyao na kufikia hadhi ya
kimataifa.
ZIFF mwaka huu
imejitolea kuwasaidia wale wote ambao wangependa kutuma maombi yao ili
kuwasaidia kufuata malekezo ya usaili, kuwapa miongozo ya uandishi wa skripti
na kuwaongezea nafasi za kuchaguliwa kuhudhuria warsha hii muhimu. Wanaotaka
kusaidiwa katika hili wanatakiwa kufika ZIFF, Ngme Kongwe Zanzibar, au kutuma
maombi yao ya kusaidiwa kwa barua pepe workshop@ziff.or.tz
Wanaotaka kujua
zaidi kuhusu warsha hii waingie kwenye tovuti hii: www.maishafilmlab.org au wawasiliane na fibby@maishafilmlab.org
No comments:
Post a Comment