Habari za Punde

Innalilaah wainnailayh rajioun Abass Ali Hassan Mwinyi Mbunge Aliyemaliza Muda Wake Jimbo la Fuoni na Mgombea wa Ubunge Fuoni

                                               
                                                 Inna lilaah wainnailayh rajioun

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi anasikitika kutangaza kifo cha Kaka yake Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi aliyefariki leo, Alhamis Tarehe 25 Septemba 2025 Jijini Zanzibar..

Ibada ya kumsalia Marehemu itafanyika katika Msikiti wa Zanzibar ( جميع ) - Msikiti wa Qaboos baada ya sala ya Ijumaa na baada ya hapo maziko yanafanyika Mangapwani katika eneo ambalo amezikwa Mzee Ali Hassan Mwinyi - ambapo watu waliopo maeneo ya Mangapwani, Bumbwini, Fujoni na maeneo ya karibu watapata kutabaruku kabla ya kuzika.

Visomo Msikitini vitaanza saa 4 asubuhi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.