Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili Unguja akitokea Pemba kufuatia kifo cha kaka yake, Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi, kilichotokea leo tarehe 25 Septemba 2025, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Marehemu Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi atazikwa kesho Ijumaa, tarehe 26 Septemba 2025, nyumbani kwao Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, mara baada ya Sala ya Ijumaa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment