Na Mwashungi Tahir na Rahma Khamis-Maelezo Zanzibar
Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kitendo kilichofanywa na Wajumbe wa Baraza la wawakilishi kupitia chama cha Wananchi (CUF) kutoka ndani ya kikao halali cha Baraza la Wawakilishi wakati wa mjadala wa kupitisha Mswaada wa sheria wa matumizi ya fedha za serikali kwa mwaka 2015/2016 ukiwa bado unaendelea.
Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema kitendo kilichofanywa na Wawakilishi hao hakikuwafurahisha kwani kinaashiria uvunjifu wa amani ulipo nchini.
Amefahamisha kuwa katika hali hiyo isiyo ya kawaida Wajumbe kutoka CUF waliamua kutoka nje ya Baraza baada ya Juma Duni Haji kuwasilisha hoja binafsi iliyodai “CUF hairidhishwi na Zoezi la uandikishaji la daftari la kudumu la wapiga kura linaloendeshwa Wilaya ya Magharibi kwa kugubikwa na udanganyifu wa kuandikisha watu wasio na sifa.
Hata hivyo Vuai amedai kuwa Madai ya CUF hayana msingi wowote na kwamba Lengo lao ni kuwazuia watu Unguja wasipate fursa ya kuandikishwa ipasavyo kwenye Daftari hilo ili kujiandalia mazingira ya Ushindi.
Aidha Vuai ametoa wito kwa WanaCCM kujitokeza kwa wingi katika Vituo vya Uandikishaji ili waweze kutimiza haki yao ya kidemokrasia.
Ameviomba Vyombo vuya Dola viweke ulinzi wa kutosha ili wananchi wote wapate haki yao ya kuandikishwa katika Daftari bila wasiwasi wowote.
Vuai amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuweza kusimamia Maendeleo ya haraka ya Zanzibar jambo ambalo limewezesha ukuaji wa uchumi na huduma mbali mbali za kijamii.
Amesema mafanikio mengine ya kupongezwa Dkt Shein ni pamoja na kusimamia Amani na utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba jambo ambalo limewezesha wazanzibar wote kushiriki katika shughuli zao za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
kutoka nje ya baraza/bunge kwa wapinzani ni jambo la kawaida kwa wapinzani duniani kote wakiona hawakubaliani au hakuna faida kuendelea kuwemo kikaoni na chama tawala huo ndio utaratibu au mfumo wa vyama vingi unavyo endeshwa,huu huwa kama mgomo baridi sasa kelele za nini Bwana Vuai,hiyo amani unayoa ashiria kuwa inavunjwa kwa kitendo chao sio kweli ni wewe binafsi huelewi haki wala mfumo huu tulio ukubali wa vyama vingi ulivyo una miiko yake ambayo huijui au huitaki umezowea mfumo wa chama kimoja ndio maana unapata shida kufanya kazi na wapinzani ndio maana mnataka kuvunjwa kwa serekali ya umoja wa kitaifa ili muweze kufanya mnavyo taka bila kuulizwa au kupingwa sasa kama mnataka hilo bora pia mrudishe pia mfumo wa chama kimoja nchini huu wa vyama vingi ccm hamuuwezi msiumize vichwa vyenu kwa kusema hakuna amani hamtaki kushindwa na nyie sio washindani.
ReplyDeletetumieni ubunifu wa kisiasa kukabiliana na kasi ya mageuzi kutoka kwa wapinzani sio siku zote kulalamika ovyo kwa kuwatia watu hofu ya kuwa tuna salama na amani pamoja na utulivu hayo yameletwa na serekali ya umoja wa kitaifa sio ccm peke yao hata hilo linawashinda kulijua?
mdau.
exccm.