Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akisoma Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha wakati wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi kupitisha Bajeti za Wizara mbelimbali za Swerikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Maofisa wa Wizara ya Fedha Zanzibar wakifuatilia Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha Zanzibar ikisomwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee katika kikao cha bajeti leo asubuhi.
Maofisa wa ZRB wakifuatilia hutubia ya Wizara ya Fedha ikisomwa wakati wa Kikao cha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016. Ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha Zanzibar.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Ali Abdalla Ali akitoka katika ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi baada ya kumaliza shighuli za Baraza baada ya kuwasilishwa Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha Zanzibar na Waziri wa wizara hiyo Mhe Omar Yussuf Mzee
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Bihindi Hamad wakibadilishana mawazo wakitoka nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa hadi jumatatu baada ya kuwasilishwa Bajeti ya Wizara ya Fedha Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akisisitiza jambo wakiwa nje ya ukumbi wa Mkutano baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa kuchgangiwa na Wajumbe katikati Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mohammed Mussa.
Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar Mhe Shamis Vuai Nahodha akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa nje ukumbi wa mkutano
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoka katika ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa hadi jumatatu kulia Mwakilishi wa Viti Maalum Mhe Marina Thomas na Mwakilishi wa Bububu Mhe Hussein Ibrahim Makungu (BHAA)
No comments:
Post a Comment