Habari za Punde

Balozi Seif ajitambulisha kwa viongozi wa kamati za siasa za CCM Mahonda

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Viongozi wa Kamati za Siasa wa Matawi Manne yaliyotoka Donge na Bumbwini kwenye Mikutano tofauti alipokwenda kujitambulisha akifafanua azma yake ya kutaka kugombea Jimbo Jipya la Mahonda nwa nafasi ya Uwakilishi.
  Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi akiwahamasisha wanawake wenzake kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura na kuichagua CCMiendelee kushika Dola na kulinda amani iliyopo nchini.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Siasa wa Matawi ya Mahonda “A”, Mangapwani , Uwandani na Zingwe Zingwe yaliyoingia katika Jimbo Jipya la Mahonda wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani alipokwenda kujitambulisha rasmi.

Picha na –OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema endapo atafanikiwa kuwa Mwakilishi wa Jimbo Jipya la Mahonda katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu atajipanga kushirikiana na Viongozi pamoja na Wananchi  katika kuona maendeleo ya haraka yanapatikana ndani ya Jimbo hilo.

Alisema aliyoyaahidi kuyafanya katika Jimbo la zamani la Kitope na kuyakamilisha  katika kipindi cha miaka kumi ya utumishi wake kasi hiyo sasa ataiendeleza kuitekeza katika Jimbo jipya la Mahonda.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa ahadi hiyo wakati wa ziara yake maalum ya kujitambulisha kwa Viongozi wa Kamati za Sioasa za  Chama cha Mapinduzi wa Matawi Manne ya  Mahonda “A “, Mangapwani, Uwandani na Zingwezingwe kwenye Mikutano tofauti.

Matawi hayo Manne yakijumuishwa na mengine Manane yaliyokuwa kwenye Jimbo la zamani la Kitope yanalifanya Jimbo Jipya la Mahonda kuwa na Matawi 12 kufuatia mabadiliko ya Majimbo yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar  kwa mujibu Katiba ya Zanzibar ya  mwaka 1984 inayotoa mamlaka kwa Tume hiyo kufanya marekebisho ya mipaka ya Majimbo kulingana na ongezeko la idadi ya watu katika kipindi  kisichopungua miaka kumi.


Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi akijitambulisha rasmi kwa wanachama wa Matawi hayo katika azma yake ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo la Mahonda alisema ameahidi kuimarisha Majengo hayo Manne ya Ofisi za Chama ili yafikie hadhi ya chama chenyewe.

“ Niliahidi mwaka 2010 kwamba ifikapo mwaka 2015 Wanachama wa Matawi yote yaliyomo ndani ya Jimbo la Kitope watafanyia Mikutano yao ndani ya Ofisi zao Mpya. Nafahari kusema kuwa  kazi hiyo nimeikamilisha kwa  zaidi ya asilimia 95%. Kazi zilizobakia kwa baadhi ya Ofisi hizo za Chama ni ndog ndogo  kama za upakaji wa rangi “. Alisema Balozi Seif.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwakumbusha wanachama wa Chama hicho kuhakikisha kwamba wanajitokeza kwa wingi kupiga kura wakati ukifika kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba.

Aliwashawishi wanachama pamoja na wananchi wote Nchini kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi  kwa kukipigia kura ili kiendelee kuongoza Dola kwa vile ndio chama pekee chenye uwezo wa kusimamia amani na utlivu uliopo hapa Nchini.

Akizungumzia mchakato wa kuwapata wagombea wateule wa CCM katika uchaguzi Mkuu kwa nafasi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Mgombea mwenzake mwenza na Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema hakuna wakati ambao CCM imepata heshima kubwa kama kipindi cha kumalizia mkutano Mkuu wa CCM wa hivi karibuni.

Alisema Wajumbe wa Mkutano  Mkuu huo na wale wa Kamati kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa pamoja na Kamati ya Maadili wamefanya upembuzi wa kuwachagua Wagombea  majembe wa kupeperusha Bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha nafasi hizo za Urais.

Alisema kazi kubwa iliyofanya na wajumbe wa Vikao hivyo inapaswa kupongezwa na Wanachama wa chama Mapinduzi  pamoja na Wananchi wote wapenda amani kwa vile wateuliwa hao wana sifa ya uwezo kamili na makini wa kuongoza Dola.

Mapema Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi  alisema Mtu anayekwenda kwa Wananchi kutafuta ajira kwa nafasi za Ubunge , Uwakilishi pamoja na Udiwani aelewew kwamba hafai kushika nafasi hizo.

Mama  Asha alisema kwa mujibu wa Katiba ya Nchi nafasi hizo zimeundwa ili wale wanaozihitaji  wafahamu kwamba kazi yao kubwa inawalazimu  kuwatumikia Wananchi waliowaomba idhini hiyo.

Aliwakumbusha na kuwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kuelewa kwamba hivi sasa wakati umefika wabadilike kukumbatia watu wasiokubali kuwatumikia.

Alifahamisha kwamba wakati wa kudanganywa kwa tabia ya 
Wananchi kupewa kitu kidogo umekwisha kwa vile mchezo huo mbaya utaendelea kuwajengea mazingira mabovu ya hatma yao ya baadaye.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi la ccm Uwandani Ndugu Haji Salim Juma kwa niaba ya viongozi wenzake amesema Wana CCM hao wamepata matumaini na faraja kutokana na msimamo wa Balozi Seif wa jitihada zake za kusimamia maendeleo ya Wananchi anaowaongoza.


1 comment:

  1. Mhe Balozi kwani muda wa kujinadi na kampeni tayari?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.