Dr Naufal K Mohammed akizungumza na Ujumbe wa Madaktari kutoka Washington Diaspora walipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kutoa huduma ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Tiba ya Meno ukiwa na Ujumbe wa Watu 17, Wamefika Ofisi hapo kujitambulisha kwa Uongozi wa hospitali
Dr Naufal K Mohammed akizungumza na Madaktari hao walipofika Ofisini kujitambulisha wakiwa na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Diaspora Zanzibar Ukiongozwa na Mkurugezi wa Idara hiyo Ndg Adila
Ujumbe wa Madaktari Madiaspora wakimsikiliza Dr Naufal K Mohammed walipofika Ofisini kwakwe kujitambulisha na kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata tiba.
Rais wa Jumuiya ya Wanawake Washington Africa Womens Cancer Awareness Association Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha Ujumbe wake aliofuatana nao Madaktari Diaspora walipofika katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kutoa huduma ya Saratani ya Matiti Kisaukari na Tiba ya Mano.
Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Washington Diaspora Asha Nyanganyi akiztowa maelezo ya Ujumbe huo kwa Dr Nawfal wakati walipofika Ofisini kwake Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja leo asubuhi kwa kutoa huduma za Meno, Kisukari kutoa dawa kwa wagonjwa na kutowa elimu ya Saratani ya Matiti kwa Wanawake Zanzibar
Dr Naufal akiwa na wageni wake akiwapeleka katika vitengo vyao vya kutowa huduma ya Afya kwa Wananchi waliofika katika hospitali ya Mnazi Mmoja kupata huduma kutoka kwa madaktari hao.
Daktari wa Kitengo cha Meno katika hospitali ya Mnazi Mmoja akitowa maelezo kwa Madaktani hao wa Fani ya Meno kutoka Washington Diaspora walipofika katika hospitali hiyo kutowa huduma ya tima ya meno kwa wananchi
Madaktari Bingwa wa eno wakiwa katika picha ya pamoja na Daktari wa Kitengo cha Meno katika hospitali ya Mnazi Mmoja.Zanzibar
Madaktari Bingwa wa Kisukari wakiwa katika Kitengo cha Kisukari katika hospitali ya Mnazi Mmoja walipofika kutoa Tiba ya Kisukari kwa Wananchi waliofika kupata huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment