Na Haji Nassor, Pemba
MWANAMKE mmoja (25), mkaazi wa
Pandani, amelazwa hospitali ya Wete Pemba, baada ya kumwagiwa maji moto na
kijana Mfaki Ali Hamad, baada ya kukataa kufanya nae mapenzi kwa muda mrefu
sasa.
Taarifa kutoka kijijini hapo zinaeleza kuwa, kijana huyo alikuwa akimfuata kwa muda mrefu mwanamke huyo aliekwenye ndoa, akitaka kufanya nae mapenzi, bila ya mafanikio na kumuahidi kumfanyia lolote.
Taarifa
hizo zinaeleza kuwa, kijana Mfaki baada ya kukataliwa na mwanamke huyo, ndipo
alipotimiza ahadi yake juzi usiku ya kumfanyishia kwa kumwagia maji moto, na
kumsababisha mauimivu makali mwilini mwake.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Sheihan Mohamed Shein alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, na kusema lilitokea majira ya saa 5:00 usiku, wakati
mwanamke huyo alipokuwa chooni akijisaidia.
Alisema
kijana huyo, aliitumia fursa ya mwanamke huyo kwenda kujisaidia usiku huo na
kufanikiwa kumwagia maji moto alioyachanganya na rangi rangi, ambapo ilionekana
mithili ya tindikali.
Kamanda
huyo wa Polisi alisema, baada ya kutokea tukio hilo mwanamke huyo alifikishwa
hospitali kwa matibabu, ambapo walikuwa na wasi wasi kwamba huwenda ni sumu
aina tindikali.
“Daktari
wa zamu wa hospitali ya Wete, alithitbitisha kuwa, hayo ni maji moto na sio
tindikali kama watu waliovyoeneza taarifa’’,alifafanua Kamanda huyo.
Alieleza
kuwa kwa mujibu wa daktari huyo, mwanamke huyo aliepatwa na ajali hiyo, amepata
mivimbe sehemu mbali mbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na mgongoni na
mapajani, ingawa hali yake inaendelea vyema.
Aidha
Kamanda huyo alisema kijana huyo, alietenda kosa hilo anaendelea kusakwa na
jeshi lake na atakapokamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Ingawa
taarifa za mwisho zinaeleza kuwa, tayari kijana huyo ameshatiwa mkononi na
Jeshi la Polisi, ambapo hili ni tukio la kwanza kwa karibu miaka mitano ya
karibuni kwa mwanamke kumwagia maji moto kwa sababu ya kimapenzi.
No comments:
Post a Comment