Habari za Punde

Mstahiki Meya wa Kinondoni Yussuf Mwenda Akabidhi Soko la Mawasiliano Simu 2000

MSTAHIKI  Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda  amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni.

Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano  kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa.

Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya kinondoni na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao.
“tumeamua kulifanya soko hili hili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza  kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri. 
 Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hio wakikagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.