Habari za Punde

Shirika la bima Zanzibar latoa msaada wa magodoro kwa Hospitali ya Chakechake

 MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar ‘ZIC’ Abdul-nassir Ahmed, akieleza azma ya shirika hilo kuendelea kusaidia taasisi za kijamii, kwenye hafla ya kukabidhi magodoro 60 kwa hospitali kuu ya Chake chake Pemba, kulia ni Mkurugenzi Masoko na Mkuu wa shirika hilo Pemba, Said Ali na kushoto ni Daktari dhamana wa hospitali hiyo Yussuf Hamad Iddi, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar ‘ZIC’ Abdul-nassir Ahmed (kulia), akimkabidhi magodoro 60 daktari dhamana wa hospitali kuu ya Chake chake Pemba, Yussuf Hamad Iddi, hafla iliofanyika hospitalini hapo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WATENDAJI wakuu wa Shirika la bima Zanzibar, ‘ZIC’ wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Abdul-nassir Ahmed mwenye suti na tai, wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa hospitali kuu ya Chake chake, ukiongozwa na daktari dhamana wa hospitali hiyo Yussuf Hamad Iddi (mwenye kofia), muda mfupi baada ya shirika hilo kukabidhi magodoro 60 hospitali hapo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar ‘ZIC’ Abdull-nassir Ahmed, akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kukabidhi magodoro 60 kwa uongozi wa hospitali kuu ya Chake chake, hafla iliofanyika hospitalini hapo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.