Habari za Punde

Taarifa za Sala ya Idd kitaifa

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                     

Kamati ya Taifa ya Sala na Baraza la Idd inapenda kukuarifu kuwa mwaka huu Sala ya Idd El Fitri Kitaifa itasaliwa katika kiwanja cha Maisara saa 1.30 na ikiwa kutanyesha mvua sala itasaliwa katika Msikiti wa Mwembeshauri na Baraza la Idd El Fitri litafanyika katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani.

Mgeni rasmi katika hafla zote mbili atakuwa Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein.

Wakati huo huo Kamati ya Taifa ya Sala na Baraza la Idd inakuarifu kuwa Sala na Baraza la Idd El Haj yatafanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Wilaya ya Kaskazini A.

Sala itasaliwa Mkokotoni katika Kiwanja cha mpira cha Sun Rise ubavuni mwa kituo cha Polisi Mkokotoni.  Baraza la Idd El Haj litafanyika Ukumbi wa Hoteli ya Lagema Nungwi.

Nakutakia maandalizi mema ya shughuli zote nne zilizotajwa  hapo juu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.