Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Abdurahamani Kasongo akitowa maelekezo ya mkutano wa kampeni kwa wagombea wa Jimbo la Kwahani wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Tawi la CCM makadara juu
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Makadara Ndg Mohammed Mussa Omar akiongoza mkutano huo wa Kampeni ya Ubunge Uwakilishi na Udiwani katika tawi la CCM makadara wilaya ya Mjini Unguja.
Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakiwa katika mkutano wa Kampeni katika viwanja vya Tawi la CCM Makadara Juu wakisikiliza utaratibu wa kampeni kwa mwenyekiti.
Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakiwa katika mkutano wa Kampeni katika viwanja vya Tawi la CCM Makadara Juu wakisikiliza utaratibu wa kampeni kwa mwenyekiti.kuaza kwa mkutano huo
Wananchi wa Tawi la CCM Makadara na Jimbo la Kwahani wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya wagombea wao wakati wakijieleza kuomba kura kwa wanaccm katika matawi
Mgombea Udiwani Wadi ya Kwahani Ndg Miza Mliwa Jecha akijieleza na kuomba kura kwa Wananchi wa Tawi la CCM Makadara na kutoa sera zake kwa Vijana kuhakikisha wanapata ajira kupitia sera ya kujiajiri wenyewe na kuwafungulia miradi wanawake wa Wadi hiyo, na kuondoa kero ya ajira katika jimbo la Kwahani Zanzibar.
Mgombea nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Kwahani Ndg Nassor Shaban Ameir, akitowa sere zake kwa wananchi wa Tawi la CCM Makadara Unguja wakati wa zoezi la mikutano ya kampeni katika Jimbo hilo. amesema ataliletea maendeleo jimbo la kwahini kupitia Elimu yake ya Uchumi
Mgombea Uwakilishi kupitia Jimbo la Kwahani Ndg Hamad Mmanga Hilika akitowa sera zake wakati wa kuomba ridhaa za Wananchi wa Tawi la CCM Makadara
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kwahani Ndg Machano Mwadini Omar akijieleza kwa Wananchi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar akiomba kura kuchagulia kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwahali anayemaliza muda wake Ndg Ali Salum Mohammed akijieleza kwa Wananchi wa Tawi la CCM Makadara Unguja wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tawi la CCM Makadara na kusema ataendeleza masendeleo ya jimbo hilo katika miradi mbalimbali ilioaza katika kipindi hichi wakati atakapo pata ridhaa za wananchi wa jimbo hilo na kuwataka watakaobahatika kupata nafasi hiyo waendeleza miradi hiyo.
Wananchi wakiwa makini kufuatilia mkutano wa kampeni ya wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani Jimbo la Kwahani Zanzibar.
Ndg Ahmeid Juma Othman, akitowa sera zake kwa wananchi wa tawi la CCM makadara wakati wa zoezi la mkutano wa kampeni kuiomba ridhaa ya wanaccm kumchagua kuliwakilisha Jimbo la Kwahani.
Ndg Abdalla Mohammed Abdalla (Teacher Dulla ) akimwaga sare zake kwa wananchi wa tawi la CCM Makadara wakati wa zoezi la mkutano wa kampeni kuomba kura ukiendelea katika matawi ya jimbo hilo mkutano uliofanyika tawi la CCM Makadara.
Wananchi wa Makadara wakifuatilia mkutano huo tawini hapo.kuwasikiliza wagombea
Wananchi wa makadara wakiwasikiliza wagombea wao wa nafasi za Ubunge Uwaki lishi na Udiwani wakijinadi kwao.
Mbunge wa Jimbo la Kwahani anayemaliza muda wake Mhe.Hussein Mwinyi akijinadi katika mkutano wa kampeni Tawi la CCM Makadara Unguja na kusema atatekeleza maadhimio yake saba aliyoyafanya katika jimbo la kwahani katika Wadi zake na shehia zake akiazia makadara shehia ilioungwanishwa na kwahani mambo hayo aliyoyatekeleza katika Wadi za Kwahani Afya Maji, Elimu kujenga skuli Michezo,timu kuhakikisha zinashiriki vizuri katika mashindano, Kuimarisha Chama cha Mapinduzi matawini Ajira kwa Vijana,Vikundi vya Ushirika kuviwezesha katika kukuza mitaji yao.
Wagombea wakifuatilia sera za wagombea wezao wakijinadi kwa wananchi wa tawi la makadara Unguja
Mgombea uwakilishi akimsikiliza muuliza swali wakati wa mkutano huo wa kampeni tawi la CCMMakadara Zanzibar.
Mgombea Ugunge Ndg Jaffar akiomba kura kwa wananchi wa tawi la ccm makadara wakati wa mkutano wa kampeni ya CCM kwa wagombea wao. 
Waheshimiwa Wagombea wakibadilishana mawazo huku mkutano ukiendelea wa kampeni ya Jimbo la Kwahani katika viwanja vya tawi la CCM Makadara juu.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo ilifuatia dua iliosomwa na mwenyekiti wa mkutabno huo
No comments:
Post a Comment