Mtandao maarufu wa social
media whatsapp huenda ukafungiwa nchini Uingereza ikiwa sheria mpya
inayojulikana kama ‘Snoopers’ Charter itapitishwa na Bunge la nchi hiyo
linaloongozwa na chama cha Conservative.
Sheria hii imo
kwenye muswada wa Sheria, Communications Data Bill
ambao uliletwa bungeni mwaka jana lakini upande wa Liberal Democrats ambao
ulikuwa serikalini wakati huo iliukataa.
Kwa kuwa Conservative
walishinda uchaguzi na kuwa na uwezo wa kupitisha muswada wowote kwa sasa kuna
uwezekano mkubwa muswada huu utaweza kupitishwa na kuwa sheria.
Sheria hii inazitaka
kampuni zinazomiliki mitandao kutunza na kuhifadhi mazungumzo ya wateja wao kwa
muda wa miezi 12 baada ya kutokea.
Kwa kuwa whatsapp, snapchat
na iMessage hutuma ujumbe kwa njia ya encyprted ambayo huwa vigumu kwa mtu
mwengine kuweza kujua kilichomo kwenye ujumbe, Serikali imesema itaweza
kutumiwa na magaidi kuweza kuwasiliana na kutumia na ujumbe bila ya
kugundulika.
Hivyo watazitaka kampuni hizi ima zibadilishe utaratibu wao
vyenginevyo zitaweza kufungiwa kwani tishio la ugaidi ni kwa maslahi ya
wananchi wengi ambao wataweza kuathirika.
No comments:
Post a Comment