Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda akiwa katika Mkutano wa Kumi wa Maspika Wanawake uliofanyika kwa siku mbili hapa Umoja wa Mataifa, Mkutano wa Maspika Wanawake, umetangulia Mkutano wa Nne wa Maspika zaidi ya 180 unaoza leo jumatatu hapa Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Kumi wa Maspika wanawake, mkutano uliojadili mbinu za kuchagiza usawa wa kijinsia, miaka 20 baada ya Beijing pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa malengo 17 ya Maendeleo Endelevu Baada ya 2015.
Na Mwandishi Maalum, New York
Mkutano wa Nne unaowakutanisha Maspika 180 na Manaibu Spika 35 kutoka nchi 140, unaanza leo ( jumatatu) hapa Makao Mkuu ya
Umoja wa Mataifa.
Mkutano
huu wa siku tatu na ambao
umeandaliwa na Chama cha Mabunge Duniani ( IPU), utafunguliwa
na Rais wa IPU Bw. Chowdhury Saber na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Matafa, Ban Ki Moon.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda anaongoza
ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu. Mkutano ambao
Maspika wanatarajiwa kujadiliana kwa kina namna ya kukabiliana na
changamoto za Amani, Demokrasia na Maendeleo kwa maono ya Kibunge.
Mkutano wa Nne wa Maspika, ulitanguliwa na Mkutano wa Kumi wa
Maspika wanawake, mkutano uliofanyika kwa siku mbili ( jumamosi na
Jumapili). Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda ameshiriki kikamilifu na kuongoza baadhi ya mikutano.
Mkutano wa
Nne wa Maspika ni sehemu ya
mfululizo wa mikutano ya Maspika hao
na ambayo imekuwa ikifanyika
kuelekea Mkutano wa Kilele wa Viongozi wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika
wiki chache zijazo ambapo watapokea na kupitisha Ajenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
No comments:
Post a Comment