STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 21.9.2015

MGOMBEA nafasi ya
urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi kujengwa
kwa hospitali mpya na ya kisasa huko Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika
mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliofanyika Bungi Miembe Mingi, Wilaya ya
Kati, Mkoa wa Kusini Unguja uliohudhuriwa na maelfu ya wanaCCM na wananchi
ambapo mgeni rasmi alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali
Mohamed Shein.
Alisema kuwa hospitali hiyo itakuwa kubwa
na ya kisasa, ambayo itakuwa na Idara mbali mbali zikiwemo Idara ya upasuaji wa
moyo, haja ndogo, saratani kwa lengo la kupunguza mzigo katika hospitali ya
Mnazi Mmoja na kuwataka wananchi kuilinda ardhi hiyo.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali hivi sasa
inatafuta Fedha kwa ajili ya ujenzi huo huku akieleza kuwa taratibu kadhaa za
awali zimeshafanyika na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Kati kwa ustahamilivu
wao kwa kuwa Wilaya hiyo bado haijapa hospitali kubwa.
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo
kueleza umuhimu wa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kueleza kuwa wapo wanaoyabeza
Mapinduzi hayo bila ya kutambua kuwa ndiyo yaliyowakomboa watu wa Zanzibar
wakiwemo wakwezi, wakulima, wavuvi na wengine wote.
Akisema kuwa Mapinduzi ndiyo yaliyoleta
muelekeo na kueleza kuwa wale wanaojifanya mahodari wa kusema kama si hayo
Mapinduzi uwezo huo wasingeliupata.
Aliwataka wananchi na wanaCCM kuzingatia
hilo na kuwaeleza kuwa wasijaribu watu
wa kuwapa uongozi na badala yake waipe CCM kuongoza nchi.
Alisisitiza kuwa hakuna mbadala wa CCM na
kwamba kama CCM isingetaka vyama vingi visingekuwepoa kwani iliamua kwa Katiba
zake zote mbili kwa maslahi ya maendeleo na lengo la kusimamisha demokrasia.
Alisema kuwa yeye anaamini sana kuwa
wananchi wote Tanzania Bara na Zanzibar wanaojua uchungu wa nchi hii na
wanaotaka maendeleo wataichagua CCM na kusema kuwa chama hicho kina uwezo wa
kuongoza nchi.
Dk. Shein alisema kuwa bado Zanzibar
inahitaji watu wenye uwezo wa kuiletea maendeleo na kusisitiza kuwa hakuna
mbadala waCCM.
Akieleza juu ya kuundwa kwa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa alisema kuwa asilimia 66 wa wananchi wa Zanzibar waliridhia kuwepo
kwa Serikali hiyo na kueleza kuwa Mfumo huo haukuja kuleta vurugu na uhasama,
kutukanana, wagombane wala kudharauliana.
Alisisitiza kuwa madhununi ya Serikali
hiyo ni kuwa na Serikali ya pamoja na kusaidiana katika kuleta maendeleo huku
akieleza jinsi ya baadhi ya vikundi vya kuvuruga amani vilivyojitokeza ndani ya
mwaka mmoja na nusu tu baada ya kuanza kazi Serikali hiyo.
Dk. Shein alisema kuwa mwenendo na mfumo
wa Zanzibar uliwekwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pamoja na mashujaa
wenzake na baada ya hapo utaratibu huo umekuwa ukifuatwa kwa kasi na kwa
malengo yale yale ya kuleta maendeleo.
Alisema kuwa watu wote wa Zanzibar
wamekuwa sawa katika Serikali ya Awamu ya kwanza na Awamu zote zilizofuata sambamba
na kuwakumbusha wananchi kuwa tangu
wakati wa ASP na hatimae CCM walijua kuwepo kwa Ilani ya uchaguzi ni jambo muhimu
sana na ndipo walipozitengeneza.
Alisema
kuwa yote yalioahidikwa katika Ilani za CCM, kwa lengo la kufanywa
yametekelezwa na kusisitiza kuwa wananchi wataichagua CCM na yeye atachaguliwa
kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi huku akiahidi
kufanya mengi kama yalivyotangulia kufanywa na chama hicho.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar inayoongozwa na CCM iliahidi kuondoa kero na katika mambo
yalioahidiwa na kufanywa kwa asilimia 90 ni suala la uwekaji wa msingi wa maji
safi na salama nchini.
Alisema kuwa katika Jimbo lililokuwa na
matatizo makubwa ya maji ni Tunguu, na kueleza kuwa juhudi kubwa zimefanywa
katika kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi na hivi sasa huduma hiyo
imekuwa ikipatikana.
Alisema kuwa tatizo la mahitaji ya maji, hayazungumzwi
tena katika Wilaya ya Kati wala Kusini, na hatua za maji Unguja na Pemba
zimechukuliwa.
Dk. Shein alisema kuwa miji ya Wete,
Chake, Mkoani na Wilaya ya Kati Zanzibar hali ya maji imeimarika, na kueleza
kuwa kipindi kijacho nguvu zitaongezwa zaidi ili kufikia asilimia 95.
Alisema kuwa ahadi zilitolewa na CCM
katika kuimarisha miundombinu ya barabara zimetekelezwa huku akieleza umuhimu
wa kujenga barabara katika sehemu za kilimo tofauti na watu wengine
wanavyodharau juhudi hizo.
Dk. Shein aliahidi kuwa Barabara
inayokwenda Jozani hadi Charawe na Jozani kwenda Ukongoroni imejengwa kwa hatua
za kifusi na katika kipindi kijacho cha miaka mitano zitatiwa lami.
Aidha, aliahidi kuwa barabara ya Umbuji
hadi Uroa itajengwa kwa kiwango cha lami hayo ndio mambo ambayo tayari yamo katika Ilani ya CCM.Aliongeza
kuwa maeneo mengi ya Wilaya ya Kati ni maeneo ya kilimo hivyo sekta hiyo nayo
itaimarisha sambamba na wakulima kuendelea kusaidiwa.
Alisema kuwa mambo 12 ya msingi
yamefanywa yakiwa pamoja na kutafuta masoko, mashamba darasa 1200, ukuaji wa
mavuno ya mpunga pamoja na juhudi nyengine za kuimarisha sekta hiyo ya kilimo
ikiwa ni pamoja na kuungwa mkono na nchi marafiki na washirika wa maendeleo
zikiwemo China na Korea.
Kwa upande wa zao la karafuu, Dk. Shein
alisema kuwa mipango aliyoifanya katika zao la karafuu ni mikubwa na asitokee
mtu kujisifu kuwa kafanya yeye bali ni Serikali chini ya uongiozi wake.
"Wengine wanataka sifa tu..”,alisema Dk. Shein
Tuliamua Serikali kuwapa fidia wakulima,
dawa za kuulia wadudu, mbolea, mbegu na
mambo mengineyo na kusema kuwa ipo haja
ya kuwasifu wakulima.
Dk. Shein alisema kuwa Wanachi wa Tunguu
wamebahatika kuwa na Chuo Kikuu katika Jimbo hilo na kueleza kuwa Chuo hicho
kitaimarishwa.
Aliendelea kueleza suala la elimu
kuendelea kuwa bure, kwa Msingi na Sekondari, na kusema kuwa kutokana na uchumi
kwenda vizuri na nia yake aliyonayo hilo litawezekana.
Alieleza kuwa hatua zinachukuliwa katika
kuimarisha uchumi wa Zanzibar ikwia ni pamoja na uchimbaji wa mafuta na kupinga
kauli za kuigeuza Zanzibar kuwa Singapore kwa siku 100.
Alisema kuwa nchi itajengwa kwa uwezo
uliopo, na na Serikali chini ya uongozi wa CCM imejiandaa kwamba Zanzibar
ikifika mwaka 2020 makusanyo yatakuwa Bilioni 800 kwa mwaka na kueleza kuwa
baada ya miaka yake mitano ya uongozi makusanyo hivi sasa ni Bil 40.5 kwa mwaka,
hivyo kwa kasi ya Ilani na kuzingatia hatua za miundombinu iliyowekwa Bandari
ya Mapigaduri itajengwa.
Alieleza pia, juhudi zinazofanywa katika
ujenzi wa jengo la uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Dk. Shein, aliomba kura kwa wananchi na
wanaCCM wote, Magufuli, Samia, Wabunge na WawakilishiTunguu, Chwaka na Uzini
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
Boresha huduma za Mnazimmoja kwanza ndio ujenge hospital mpya
ReplyDelete