Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali iddi amesema CCM
imegundua kuwa upotoshaji anaoufanya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif
katika mikutano yake ya kampeni ni janja yake ya kujaribu kuwapa moyo wanachama na
wafuasi wa chama hicho ambao tayari wameonesha kukata tamaa.
Balozi
Seif ambaye ni Makamu wa Pili
wa Rais aliwaambia wananchi waliohudhuria mkutano wakampe ni huko Bungi Wilaya Kati kuwa
Maalim Seif ambaye ni mgombea urais kupitia chama cha CUF hana kipya cha
kuwaeleza wafuasi wake
hivyo analofanya hivi sasa kila akisimama majukwani ni kusema uongo ili kujaribu kuwapa moyo baada kuona wamekata tamaa na
ushindi.
“Maalim
acha kuwadanganya wanachama na wafuasi wako, CCM hawadanganyiki na
ghiliba zako mwaka huu ndio mwaka wa kuizika CUF”alielezaBalozi Seif.
Balozi
Seif alisema Maalim Seif na CUF yake hawana sifa za kuongoza na
kuwataka wasahau kuingiaIkulu.
“Nia
ya kushinda tunayo,
hatujawahi kushindwa, dhamira ya kushinda tunayo na sababu za kushinda tunazo”alisisitiza Balozi
Seif.
NAIBU KATIBU MKUU CCM: CUF IMECHEMSHA, HAINA ILANI
Chama
cha Wananchi-CUF
kuzindua kampeni za uchaguzi bila ya Ilani ni kielelezo tosha kuwa chama hicho kimekosa umakini wa uongozi hivyo hakipaswi kupewa fursa ya kuongoza nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai aliwaambia wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika Bungi Wilaya ya
Kati Mkoa wa Kusini kuwa chama cha CUF baada ya kuoneshewa kidole na
baadhi ya wananchi kwa kukosa Ilani harakaharaka kilikurupuka na kuandaa Ilani na
kuizindua juzi.
Matokeo ya kukurupuka huko Vuai alibainisha kuwa chama hicho kimejikuta kikinakili Ilani ya Uchaguzi ya
CCM kwa kubadilibadili kurasa tu.
Alifafanua kuwa vyama makini kwa uongozi vimekuwa vikiandaa Ilani zake zinazogusa kila sehemu ya maisha ya mwananchi wakati wa chaguzi zote kama ilivyofanya
Afro Shirazi wakati wa chaguzi za kutafuta Uhuru hadi hivi sasa CCM kuendeleza nchi.
Ilani hizo ndio zinazowavutia wananchi na kukichagua CCM kushika dola wakati wote.
Ilani ya
ASP katika mkutano wa mwisho wa kampeni uliofanyika Kisiwandui Unguja
ilieleza kuwa elimu na matibabu itatolewa bure na
ndio maana ilishinda uchaguzi japoku walifanyiwa ghiliba na kunyimwa kuongoza nchi.
SHAMSI:MAALIM SEIF HANA DHAMIRA WALA NIA YA
KUINDELEZA ZANZIBAR
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM Shamsi Vuai Nahodha amesema Maalim Seif Sharif Hamad
hana dhamira wala nia ya kuindeleza Zanzibar na kwamba kauliza kuibadili Zanzibar
ndani ya siku mia moja endapo atakuwa Rais ni ghiliba za kisiasa tu kupata kura.
Alifafanua kuwa miaka tisa ya
Maalim Seif kuwa katika madaraka makubwa kwa nyakati tofauti katika Serikali ya Zanzibar
ameshindwa kuleta mbinu au mpango wa kuifanya Zanzibar kama nchi ya Singapore.
“Alikuwa
Waziri Kiongozi kwa miaka 4 huku akipewa mamlaka makubwa na Rais wa wakati huo marehemu
Mzee Abdulwakil na baadae hivi sasa miaka mitano akiwa Makamu wa Kwanza
wa Rais hajafanya lolote”Alieleza Shamsi na kusisitiza kuwa kama miaka tisa ameshindwa ataweza siku mia moja.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alieleza kuwa inaonesha kiongozi huyo anazeeka vibaya kwa kuwa hata huo uumini
wake wa demokrasia una mashaka kwa kuwa yeye mwenyewe anashindwa kutekeleza.
“Mbona kama ni muumini wa demokrasi ya Uingereza mbona haifuati?
Mbona wenzake wakishindwa uchaguzi mara moja tu hujiuzulu lakini yeye anashindwa uchaguzi anaendelea kung’ang’ania”
alisisitiza Shamsi.
Aliwaeleza mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa kiongozi huyo ambaye ni Makamu wa
Kwanza wa Rais kupita akiwaeleza wananchi kuwa serikali haijafanya kitu zote hizo ni ghiliba ambazo wananchi wanapaswa kuwa makini
na kutompa nafasi yoyote yeye na chama chake.
No comments:
Post a Comment