STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 3.8.2015

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za rambirambi Makamu
wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) na Mfalme wa Dubai,
Sheikh Mohammed bin Rashid Al-Maktoum kufuatia kifo cha mwanawe Sheikh Rashid
bin Mohammed Al- Maktoum.
Katika salamu hizo za rambirambi, Dk. Shein alisema kuwa kwa niaba yake, Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wa Zanzibar wanatoa mkono wa pole
kufuatia kifo hicho.
Aidha, salamu hizo za rambirambi zilimuombea Dua kwa MwenyeziMungu Kiongozi
huyo wa UAE pamoja na Wanafamilia wa Al-Maktoum na kuwaomba kuwa na subira
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.
Dk. Shein amemuomba Mwenyezi Mungu kuilaza roho ya marehemu mahala pema
peponi, Amin.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment