STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 14 Septemba , 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Ndg. Mwinyiussi Abdalla Hassan.
Ndugu Mwinyiussi anakuwa Mkuu wa Wilaya wa kwanza wa wilaya hiyo mpya ambayo iliundwa mwezi Mei mwaka huu kufuatia mabadiliko ya kiutawala ambapo iliyokuwa Wilaya ya Magharibi katika mkoa wa Mjini Magharibi iligawanywa kuwa wilaya mbili-Magharibi ‘A’ na Magharibi ‘B’
Katika mabadiliko hayo Mheshimiwa Rais alimteua pia Ndg. Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘B’ambaye alimuapisha tarehe13 Mei, 2015.
Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mwinyiussi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheri.
Wengine ni Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji Khamis, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdulla Mwinyi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abdulrahman Khatib.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822
No comments:
Post a Comment