Habari za Punde

Rais Kikwete aagwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo



Askari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete alipoagwa rasmi na Vikosi hivyo leo,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi la Vikosi vya  Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  kumuaga kwa kumaliza muda wake wa Urais leo.[Picha na Ikulu.]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo,[Picha na Ikulu.]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (wan ne kushoto) akiwa na Viongozi wengine wakisimama kupokea salamu ya heshma ya kwaride la Vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa ulipopigwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa rasmi leo,[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.