Habari za Punde

Shamrashamra za Uzinduzi wa Umeme Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani Pemba



Wakaazi wa Kisiwa cha Kisiwa Panza Wila ya Mkoani Pemba wakiwa katika ufukwe wa Kisiwa hicho wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya Uzinduzi wa Mradi wa Umeme kwa wakazi wa Kisiwa hicho uliopita chini ya Bahari ukitokea Chokocho hadi kisiwa panza. 
Wanakamati ya Maendeleo ya Kisiwa Panza wakiongozwa na Sheha Mstaaf na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Mzee Faki Ali Faki wa kwanza, wakimsubiri Rais wa Zanzibar kumpokea wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Umeme katika kisiwa hicho kutowa huduma hiyo kwa Wananchi wake kilikuwa hakina umeme karibu miaka yote.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili na Boti katika Kisiwa Panza tayari kwa uzinduzi wa Umeme uliopita bahari kutokana na juhudi za Shirika la Umeme Zanzibar kuweza kufikisha umeme katika Kisiwa hicho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kisiwa Panza Mzee Faki Ali Faki wakati alipowasili katika Kisiwa hicho kwa ajili ya Uzinduzi wa Umeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa Kisiwa Panza alipowasili kisiwani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mzee wa Kisiwa Panza baada ya kuwasili katika kisiwa hicho kwa ajili ya Uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Umeme kisiwani huno.
Eneo uliopita Umeme huo ukitokea Chokocho hadi Kisiwa Panza 
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Ndg Hassan akimuenesha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, eneo uliopita Umeme huo wakati wa Uzinduzi wake katika Kisiwa Panza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Ndg Hassan mwenye suti baada ya Uzinduzi wa Umeme huo akielekea Jukwaa kuu kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi wa Kisiwa Panza. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahomed Shein, kulia Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Ndg Hassan na Waziri wa Ardhi Maji na Makaazi Mhe Ramadhin Abdalla Shaban na kulia Mkuu wa Mkoa Mhe Mwanajuma Majin na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mhe Mustafa Aboud Jumbe wakishangilia baada ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme katika kisiwa Panza.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibar wakifuatilia uzinduzi wa Mradi huo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,wakiwa katika viwanja vya mpira kisiwa Panza.
Wazee wa Kisiwa Panza wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akiwahutubia baada ya kuwazindulia Umeme kwa ajili ya Wananchi wa Kisiwa hicho.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Ndg. Hassan akitowa maelezo ya Mradi huo wa kusambaza Umeme kupitia Bahari hadi Kisiwa Panza wakati wa uzinduzi huo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Viongozi wa Serikali wakiwa katika viwanja vya mpira Kisiwa Panza wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mradi Umeme Kisiwa Panza, wakati Rais wa Zanzibar akiwahutubia Wananchi wa Kisiwa hicho. 
Mafundi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakifuatilia hafla hiyo wakati wa Uzinduzi wa Umeme katika Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Kisiwa Panza wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Umeme kisiwani humo.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme wakiwa katika hafla hiyo.
Mwananchi wa Kisiwa Panza akiwa katika viwanja hivyo akifuatilia uzinduzi huo wa Umeme Kisiwani mwao.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa Kisiwa Panza baada kumaliza kwa hafla ya Uzinduzi wa Umeme Kisiwa Panza Wila ya Mkoani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa Kisiwa Panza baada kumaliza kwa hafla ya Uzinduzi wa Umeme Kisiwa Panza Wila ya Mkoani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa Kisiwa Panza baada kumaliza kwa hafla ya Uzinduzi wa Umeme Kisiwa Panza Wila ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Kisiwqa Panza wakiwa katika ufukwe huo wakimuaga Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Umeme Kisiwa Panza. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot, Zanzinews.com.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.