WANAFUNZI waskuli mbali mbali kisiwani Pemba,
wakipitia kwa makini maelezo yanayoelezea jinsi ya kutumia vyakula vya matunda
na mboga mboga, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Jumuiya ya
wanafunzi wa Tanzania waliosoma Japani(JATA).(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
KAIMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania
waliosoma Japani (JATA) Mbarouk Talib, akizungumza na wanafunzi wa skuli mbali
mbali za Sekondari kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa Fidel Castro.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Mkurugenzi Mkaazi wa
JICA Tanzania Mhe: Toshio Nagase, akizungumza na wanafunzi wa skuli mbali mbali
za sekondari kisiwani Pemba, huko katika skuli ya Fidel Castro juu ya
kuhamasisha utumiaji wa vyakula vya mboga mboga na matunda .(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
KATIBU Tawala Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Ahmed Khalid
akifungua warsha ya siku moja kwa wanafunzi wa skuli za sekondari kisiwani
Pemba, huko katika skuli ya Fidel Castro juu ya uhamasishaji wa utumiaji wa
vyakula vya mboga mboga na matunda.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
KATIBU Mtendaji wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania
waliosoma Japani (JATA) Selina
Lyimo, akitoa neon la shukurani kwa mgeni rasmi baada ya kufungua warsha hiyo
ya siku moja kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Idara ya Kinga
Wizara ya Afya Pemba dk. Shaibu Itibar, akiwasilisha mada ya Virutibisho katika
warsha ya siku moja, iliyowashirikisha wanafunzi mbali mbali kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MRATIBI wa kitengo cha kilimo cha Umwagiliaji kwa
kutumia matonye ya maji, kutoka JICA Tanzania Hideyuki Morri, akiwasilisha mada
ya umwagiliaji kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WANAFUNZI wa skuli mbali mbali kisiwani Pemba
wakiuliza maswali, juu ya uendelezaji wa kilimo cha mboga mboga na matunda,
kupitia mradi wa Umwagiliaji maji uliobuniwa na wanachama wa JATA Tanzania.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa wanachama wa JATA Tanzania akiwafahamisha wanafunzi namna ya kilimo cha umwagiliaji maji kwa kutumia matonye inavyofanya kazi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment