Habari za Punde

Wananchi walivyopiga kura kwa amani na utulivu Pemba

 KARANI wa tume ya Uchaguzi Zanzibar akimkatia karatasi ya kupigia kura Mzee Hamad Salim Faki mmoja wa wananchi aliyefika katika kituo cha kupigia kura katika Shehia ya Pembeni Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba.(Picha na Bakari Mussa, PEMBA.)
 Mzee Hamad Salim Faki Wananchi aliyejitokeza kupiga kura akiiangalia kwa makini majina ya wagombea wa Urais ili kuweza kumchagua kiongozi anayemtaka, kama alivyo kutwa na mpiga picha wetu katika kituo cha Shehia ya Pembeni Wilaya ya Wete.(Picha na Bakari Mussa, PEMBA.)
 WANANCHI mbali mbali wakiwa katika foleni wakisubiri zamu zao kuingi na kwenda kupiga kura katika kituo cha skuli ya Shengejuu Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba.(Picha na Bakari Mussa, PEMBA.)
 WATU wenye Ulemavu nao hawakuwa nyuma na kuipoteza haki yao ya kupiga kura, baada ya kupatia taaluma hiyo na kuhamasika, Pichani mmoja mama mweye Ulemavu akiwa na kibaskeli chake na Mwanawe akisubiri kwenda kupiga kura katika kituo cha shengejuu jimbo la Kojani Wilaya ya Wete.(Picha na Bakari Mussa, PEMBA.)
 LICHA ya Mvua iliyokuwa ikinyesha katika baadhi ya maeneo ya kisiwa Cha Pemba, lakini wananchi hawakuweza kuipoteza haki yao, pichani wananchi wakiwa katika foleni wakisubiri kwenda kupiga kura katika ya Wambaa jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani.(Picha na Haji Nassor, PEMBA.)
 WAKALA wa Chama cha ADA-TADEA kutoka jimbo la Bububu, ambaye ametolewa nje na watendaji wa Tume ya Uchaguzi katika kituo cha skuli ya Wambaa Jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani, akiwa na lengo la kusimamia kura za mgombea urais wa chama hicho, nyuma yake ni Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo, Mohamed Mbwana Hamad.(Picha na Haji Nassor, PEMBA.)

 MGOMBEA wa Ubunge wa Jimbo la Chambani Mhe;Yussuf Salim Hussein, akikagua zoezi la Upigaji wa kura katika kituo cha skuli ya Wambaa Jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani.(Picha na Haji Nassor, PEMBA.)
KIJANA mmoja akimsaidia mama mtumzima katika kuweza kuitumia haki yake ya kupigia kura, mara baada ya kufika katika kituo cha skuli ya Wambaa jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani.(Picha na Haji Nassor, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.