Mmoja wa wafanyakazi wa Chama
Cha Albino, Christina Mbedi akielezea namna Chama cha Albino kinavyofanya
kazi zake kwa Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale
wakati wa ziara ya viongozi wa Zantel ofisini kwao. Anayetizama kulia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Albino Tanzania, Ernest Kimaya.
Meneja wa Chapa na Mawasiliano
wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa vifaa vya mawasiliano kwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino Tanzabua, Ernest Kimaya.
Wanaotazama nyuma ni baadhi ya viongozi wa Chama cha Albino.
Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel,
Arnold Madale akikabidhi msaada wa vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa
Umoja wa Chama cha Albino Tanzania, Ernest Kimaya. Anayetazama nyuma ni
mmoja wa viongozi wa Chama cha Albino.
Viongozi wa Chama cha Albino na
Zantel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Viongozi wa Zantel
kutembelea ofisi zao.
- Yaiunganisha ofisi ya
chama cha albino na huduma ya mtandao pamoja na mawasiliano ya simu
Dar
es Salaam, 8/10/2015:
Uongozi wa Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo umetembelea ofisi za Chama
cha Maalbino Tanzania, ziara yenye lengo la kujifunza zaidi kuhusu Chama cha
Maalbino kinavyofanya kazi pamoja na kuboresha ushirikiano baina yao.
Pamoja na kuzungumza na
viongozi wa chama cha Maalbino, uongozi wa Zantel pia umekabidhi huduma za
simu, kwa kuwapa namba maalumu pamoja na kuwaunganisha na huduma ya mtandao.
Akizungumza wakati wa ziara
hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress Chissenga alisema huu ni
mwendelezo wa ushirikiano baina ya Zantel na Chama Cha Maalbino.
‘Leo tumeamua kuja
kuwatembelea wenzetu wa Chama cha Maalbino ili kujionea namna wanavyofanya
kazi, na msaada huu wa intaneti pamoja na huduma ya simu tuliyokabidhi leo
itawawezesha viongozi na watendaji wa chama cha albino kupiga simu bure kwa
mwaka mzima, lakini pia itarahisisha mawasiliano baina yao na viongozi wengine
wa chama kutoka mikoani’ alisema Chissenga.
Katika ziara hiyo, viongozi
wa Zantel na Chama cha Maalbino Tanzania walijadiliana maeneo mengine ya
kuongeza ushirikiano baina yao katika kuhakikisha chama cha Maalbino
kinatekeleza majukumu yake zaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Chama cha Albino Tanzania, Bwana Ernest Kimaya, alisema wanaishukuru kampuni
ya Zantel kwa kuendelea kuwaunga mkono katika juhudi zao za kuhakikisha mauaji
ya albino yanamalizika nchini.
‘Tunawashukuru Zantel kwa
kuendelea kutuunga mkono na msaada huu waliotukabidhi leo, unaonyesha kuwa wana
nia ya dhati ya kushirikiana na chama chetu’ alisema Kimaya.
Ziara
hii ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel
na Chama cha Maalbino Tanzania, ambao ulilenga kusambaza elimu juu ya ulemavu.
No comments:
Post a Comment