Habari za Punde

Kamanda Mpinga Azindua Operesheni Paza Sauti,Jijini Dar es Salaam.leo

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP  Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
 Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari  zake mkoani wakati wa  kuzindua  wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona  viashiria vya uvunjifu wa sheria za  barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua  Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa  wanapoona kuna viashiria vya  uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.
(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

1 comment:

  1. Kutupa Maelezo marefu yasio na maana haifai kitu kusaidia wanamchi tunaomba namba au mawasiliano ya kamanda mpunga yawepo kwa maoni na matatizo ya Askari wa barabarani wasio wajibika

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.