Habari za Punde

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Zanzibar Yamuaga Mkurugenzi Wake kwa Michezo Mbalimbali katika Hoteli ya Kigaeni

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Tanzania NIDA Afisi ya Zanzibar Ndg Vuai Mussa Suleiman akiwahutubia Wafanyajkazi wa NIDA wakati wa hafla ya kuagwa baada ya kumaliza Utumishi wake katika Mamlaka hiyo kwa michezo mbalimbali iliofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Kigaeni Zanzibar.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Ndg Vuai Mussa akishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba ikiwa ni moja ya michezo iliandaliwa katika hafla hiyo ya kumuaga iliofanyika katika ufukwe wa hoteli ya kigaeni Makunduchi Zanzibar.
Mchezo wa Kufuta kamba ukiwa unaendelea ikiwa ni shara shara za kumuaga Mkurugenzi wao.
Hariyapuuuuuu futa futa............
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulishi vya Taifa NIDA Tanzania Ndg Vuai Mussa Suleiman, akifurahia baada ya kumaliza kwa uvutaji wa kamba na Wafanyakazi wake.  
Hayaa  hariyapuuu......... futa  futa .......... mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake ukiendelea katika sherehe hizo za kumuaga Mkurugenzi wao katika ufukwe wa hoteli ya Kigaeni Makunduchi Zanzibar.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho wakishiriki mchezo wa mpira wa Vall Ball 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho wakishiriki Mchezo wa Resi za Magunia 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho wakishiriki Mchezo wa Resi za Magunia 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho wakishiriki Mchezo wa Resi za Magunia 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakishiriki katika nmchezo wa Bao la gete ikiwa ni shamra shamra za kumuaga Mkurugenzi wao baada ya kumaliza Muda wa Utumishi wake katika NIDA.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Tanzania NIDA wakishiriki katika mchezo wa kupiga shabaha kwa kutumia panda, (Manati) 
Mfanyakazi wa NIDA Zanzibar akilenga shabaha kwa kutumia Panda (Manati) 
Wafanyakazi wa NIDA Zanzibar wamshangilia mshindi wa mchezo wa kupiga shabaha kwa kutumia Panda (Manati) baada ya kuibuka mshindi wa mchezo huo,





Wafanyakazi wa NIDA Zanzibar wakiwa na Kombe lao la ushindi kwa kuvuta kamba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.